Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dua William Nkurua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. WILLIAM D. NKURUA aliuliza:- Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu kinatumia majengo ya nyumba za kuishi Askari Polisi:- Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Nanyumbu?

Supplementary Question 1

MHE. WILLIAM D. NKURUA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote nitoe shukrani zangu kwa Serikali kwa sababu Wilaya yetu ya Nanyumbu pia tulikuwa na matatizo ya usafiri kwa Jeshi la Polisi lakini siku za hivi karibuni Serikali imetupatia na sasa polisi wana uwezo wa kufanya kazi kiurahisi. Hata hivyo, pamoja na shukrani hizo, nataka niongeze swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekiri kwamba Nanyumbu ni miongoni mwa wilaya mpya na hatuna jengo lenye hadhi ya kuwa na hadhi ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya. Sasa kwa kuwa Serikali inajua hilo.

Je, nitarajie sasa kwenye bajeti ijayo kuona haya maandalizi ambayo Serikali imesema ipo katika maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho; je, kwenye bajeti hii ijayo nitarajie kuona hiyo bajeti inasomwa? Ahsante.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa William Dua, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie kwamba kama ambavyo alivyokuja kulizungumzia suala la mapungufu ya usafiri na tukalifanyia kazi, basi na suala la kuhakikisha kwamba tunafanya kila linalowezekana ili kuimarisha kituo cha polisi katika Wilaya ya Nanyumbu nacho vilevile tutachukulia kwa uzito kama ambavyo tumechukulia uzito wa suala la changamoto ya gari katika wilaya yake.