Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Katika Jimbo la Nyang’hwale kuna maeneo mengi sana ya Wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu kama vile Isakeli, Isonda, Lyulu, Nyamalapa, Lubando, Shibalanga na Kasubuya ambayo Wachimbaji hao wanafanya kazi na Dhahabu inapatikana bila utaratibu wowote? (a) Je, ni lini Serikali itayarasimisha maeneo hayo na kuyagawa kwa Wachimbaji ili watambulike Kisheria na iwe rahisi kwa Serikali kukusanya kodi? (b) Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake iliyoitoa mbele ya Waziri Mkuu ya kulitoa eneo la Bululu kwa Wachimbaji wadogo?

Supplementary Question 1

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri na Naibu Waziri na Watendaji wote wa Wizara kwa kutoa leseni 22 kwa wachimbaji wadogo wa Wilaya ya Nyang‟hwale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali kwa kuwa Wachimbaji wengi bado wako maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Nyang‟hwale kama vile Isekeli, Isonda, Lyulu, Nyamalapa, Ifungandi, Shibalanga pamoja na Kasubuya, Je, Wizara imejipanga vipi kuwapa tena maeneo hayo wale Wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali imeshatoa leseni kwa Wachimbaji wadogo eneo la Bululu hivi karibuni uzalishaji wa dhahabu nyingi zitaanza kutoka lakini kuna jengo ambalo liko tayari kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu. Je Serikali iko tayari sasa kukamilisha vibali vyote ili kufungua Jengo hilo la ununuzi wa dhahabu Wilaya ya Nyang'hwale? (Makofi)

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa katika majibu ya swali la msingi sisi kama Wizara ya Madini kwa kupitia Tume ya Madini tunaendelea kuhakikisha kwamba yale maeneo yote tunayoyaona kwamba yana madini ambayo wachimbaji wadogo wanaweza wakachimba basi sisi hatuhusiki kabisa kuwapa wachimbaji wadogo na kuchimba na hata katika majibu yangu ya msingi nimetoa wito kwa wale Wamiliki wote wanaomiliki maeneo makubwa ya utafiti na hawayaendelezi yale maeneo na utafiti hauendelei.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Serikali tuko tayari kuyafuta maeneo hayo, kufuta leseni hizo za utafiti na kuwapa wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba, waweze kulipa Kodi na wao wenyewe waweze kujikimu katika maisha yao. Vilevile niendelee kumshukuru sana Mbunge kwa jinsi anavyofatilia na jinsi anavyokuwa karibu na wachimbaji wadogo katika Jimbo lake kwa sababu tunatambua Jimbo lake lina wachimbaji wadogo wengi sana.

Mheshimiwa Spika, nimuhakikishie katika swali lake la pili ameuliza utayari wa sisi Wizara na Tume ya Madini kuanzisha soko kwa ajili ya kuuza madini katika Jengo ambalo liko tayari nimueleze tu Mheshimiwa Mbunge sisi tuko tayari na sasa hivi nawaagiza Tume ya Madini waende katika Jengo hilo wakague kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa eneo hilo au wa Wilaya ya Nyang‟hwale walione kama linatimiza vigezo mara moja soko hilo lifunguliwe na madini yaanze kuuzwa katika soko hilo. (Makofi)