Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:- Viongozi wa Kitaifa wanaofanya ziara Tanzania walikuwa wakifika Zanzibar na kuonana na Rais wa Zanzibar:- (a) Je, kwa nini katika siku za karibuni viongozi hao wamekuwa wakiishia Tanzania Bara? (b) Je, ni viongozi wangapi wa Kimataifa ikiwemo Marais ambao wamefanya ziara Tanzania katika kipindi cha 2016/2017 na nchi wanazotoka? (c) Je, kati ya viongozi hao wangapi wamefika Zanzibar na wangapi hawakufika na kwa sababu gani?

Supplementary Question 1

MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru sana kwa majibu hayo mazuri ya
Mheshimiwa Waziri lakini je, Serikali ya Muungano au Wizara hii ya Mambo ya Nje inazishauri zile nchi wakati zina mpango wa kuja kutembelea Tanzania kuziarifu kuwa nchi yetu ya Tanzania ina sehemu mbili za Muungano na kila sehemu ina mahitaji yake ya kiuchumi. Hivyo basi, Wizara ingekuwa inazishauri kwa sababu ukiangalia nchi tisa tu ambazo zimekuja Zanzibar naamini zingekuja na hizi nchi nyingine 12 kuna fursa nyingi ambazo ziko Zanzibar ambazo bara hakuna na kuna fursa ambazo ziko bara ambazo Zanzibar hakuna.

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Wizara iweze kuzishawishi wakati nchi za nje zinapoweza ku-engage kuja Zanzibar kuja kutembelea Tanzania. Basi iziambie kuwa Tanzania ina nchi mbili na nchi hizo mbili kila upande una vipaumbele vyake vya kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ambalo nataka niliseme, Wizara inafanya jitihada gani kuwashawishi wale viongozi ambao hawakuja Zanzibar kutembelea wakati wa ziara zao lakini kufanya ushawishi wakutane na viongozi wa Zanzibar huku Tanzania Barai ili wale viongozi wa Zanzibar waweze kutoa haja zao na kuweza kutoa ushahwishi wao wa kuiona Zanzibar nayo inanufaika na ugeni ule. Ahsante sana.

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, nchi yetu ni nchi moja kwa mujibu wa Ibara ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Na masuala ya nje ni sual ala Muungano kwa m ujibu wa Ibara ya 4 nyongeza ya kwanza ya Katiba. Kwa hiyo, uhusiano wetu na mambo ya nchi za nje unachukulia maanani suala la kwamba ni nchi moja.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mahusiano yetu mara nyingi tukiwasiliana wanafahamu kwamba kuna nchi moja inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja na hayo, Serikali na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje imekuwa ikifanya jitihada kubwa sana kuhakikisha kwamba kwa sababu ya historia ya Muungano wetu na hali halisi kwamba ni Muungano ambao umetokana na nchi mbili tunahakikisha ya kwamba wakati viongozi hao wanapokuja nchini, tunajenga ushawishi mkubwa ili watembelee Zanzibar na ndiyo maana kuanzia 2015 mpaka sasa viongozi 21 waliotembelea nchini kwetu. Tisa kati yao wametembelea Zanzibar, vile vile ifahamike kwamba kuna wengine vile vile ambao wametembelea Zanzibar tu wala hawajatembelea upande mwingine wa Jamhuri.

Mheshimiwa Spika, naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kati ya masuala ambayo yanapewa kipaumbele sana katika uhusiano wa Kimataifa ni Muungano wetu ndiyo maana hata kwenye Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kuna Idara maalum inahusika na mambo ya Zanzibar. Mualiko wowote au kiongozi yeyote akija ushawishi mkubwa unafanyika ili aweze kutembelea pande zote mbili za Muungano.

Mheshimiwa Spika, sasa mara nyingi kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi mara nyingine linakuwa ni suala la utashi wa kiongozi mwenyewe na hauwezi kumlazimisha. Kwa hiyo, nimueleze tu kwanmba kwa kweli Serikali inajitahidi sana kuhakikisha kwamba viongozi hawa wanapata fursa ya kutembelea maeneo yote na hasa kujaribu vile vile kuelezea kuhusu fursa za kiuchumi na za kitalii zilizopo Zanzibar.