Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:- Kuna baadhi ya Askari Polisi kupandishwa vyeo lakini hawapati stahili zao kama inavyotakiwa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari hao stahiki zao?

Supplementary Question 1

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Mpaka sasa hivi Mkoa wa Njombe kuna tatizo kubwa sana la kuuawa watoto wadogo. Sasa Serikali inasemaje kuhusiana na hili, maana wananchi wa Njombe sasa hivi wana wasiwasi mkubwa na wazazi wanawapeleka watoto wao shuleni. Je, Serikali inasemaje kuhusiana na mauaji haya yanayoendelea katika Mkoa wa Njombe?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kumekuwa na sintofahamu na kuzuka kwa taharuki katika Mkoa wa Njombe kutokana na vitendo vya baadhi ya Watanzania wenzetu ambao wamekuwa wakiwachukua watoto wadogo na kuwaua. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kuanzia juzi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Injinia Hamad Masauni yuko kule Mkoa wa Njombe anafanya vikao na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya pamoja na Mkoa kuhakikisha kwamba vitendo hivi vinakomeshwa, lakini taarifa za awali zinaonesha ni imani za kishirikina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wabunge watupe ushirikiano
kwa sababu Waheshimiwa Wabunge maeneo yale wanayafahamu vizuri. Nitoe onyo siyo kwa Njombe peke yake bali kwa Watanzania wote kwamba wasitingishe kiberiti cha Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, wasipoacha vitendo hivyo watakipata cha mtema kuni na tunaanza na kule Njombe ambako tumeshabaini majina kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria.

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:- Kuna baadhi ya Askari Polisi kupandishwa vyeo lakini hawapati stahili zao kama inavyotakiwa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari hao stahiki zao?

Supplementary Question 2

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimpongeze sana Mheshimiwa muuliza swali Mheshimiwa Mwatum Dau. Kwa kweli hawapati stahili zao Polisi na waliojenga Vituo vya Polisi pamoja na Ofisi zao. Swali la Msingi linahusiana na kwamba hawapati stahili zao, karibu mwaka wa sita au wa saba….

MWENYEKITI: Swali swali.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili limeahidi kwa kampuni ya Albertina kumlipa pesa zake milioni 200 kwenye bajeti iliyopita ya nyuma yake na mpaka leo hajalipwa na Mheshimiwa amekuwa akitembea na ilani ya chama cha Mapinduzi. Je, ni lini stahili hizi atapata kwa ajili ya kituo hiki cha…

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Jaku amekuwa akifuatilia sana suala la huyu Askari ambaye amezungumzia. Nimuhakikishie kwamba yale ambayo nimeyajibu kwenye swali la msingi, huyu anayemsema ni baadhi ya wale Askari ambao wako katika hatua za mwisho mwisho kumaliza matatizo yao. Ni kweli kabisa katika Ilani hii ya CCM, Ibara ya 146 imezungumzia stahiki za askari na ndiyo maana sisi kama Wizara tunawajibika kuhakikisha kwamba stahiki za askari hazichezewi kwa namna yoyote ile.

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:- Kuna baadhi ya Askari Polisi kupandishwa vyeo lakini hawapati stahili zao kama inavyotakiwa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari hao stahiki zao?

Supplementary Question 3

MHE. MWATUM DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa jibu lake zuri ambalo alilolitoa hapo, lakini naomba kuuliza swali la langu la nyongeza. Tunaelewa kuwa Serikali inawajibika vilivyo katika kushughulikia na kutatua matatizo hayo. Je, ni lini hasa Serikali itafikia ukomo wa suala hili kwa kuwa imekuwa ni kero kubwa kwa Askari wetu, kwani kufanyiwa hivyo pia kunawanyima haki zao na vilevile itawapelekea kutokufanya kazi kwa ufanisi na uadilifu? Ahsante.

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi ni kwamba Maofisa, Wakaguzi pamoja na Askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na hata vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vilivyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mishahara yao inaendelea kurekebishwa. Hata hivyo, pale ambapo kutorekebishwa kwa mshahara kwa askari yeyote kutatokana na uzembe wa makusudi kwa Afisa ambaye anashughulika na mishahara ya Askari nimeshatoa maelekezo kwamba ifikapo mwezi wa Tano mwaka huu asiwepo Askari, wala Afisa wala Mkaguzi anayelalamikia stahiki yake. Pia nimewaelekeza kwamba wasicheze na maslahi na stahiki za Askari. Kufanya hivyo ni sawa na kushika mboni ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Name

Venance Methusalah Mwamoto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:- Kuna baadhi ya Askari Polisi kupandishwa vyeo lakini hawapati stahili zao kama inavyotakiwa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari hao stahiki zao?

Supplementary Question 4

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize swali moja tu dogo la nyongeza. Kwa kuwa tunazungumza habari za stahiki za Maaskari Wilaya ya Kilolo toka imeanzishwa sasa hivi takribani miaka 17 Askari wamekuwa wakiahidiwa kuwa na Ofisi ya Wilaya ya Kilolo na nyumba za Maaskari, mpaka leo ni kila mwaka tumekuwa tukiahidiwa. Sasa nataka nijue kutokuwa na nyumba na Ofisi si wanakosa stahiki zao la halali?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Venance Mwamoto kwa jina la utani mzee wa vinungu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba siyo Jeshi la Polisi pekeyake tuna tatizo la ofisi pamoja na makazi kwa Askari. Hata hivyo, nimhakikishie kwamba tunaendelea kutenga fedha ili kupunguza kama siyo kumaliza kabisa suala la makazi na ofisi kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Nitumie fursa hii pia kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekuwa akitupatia fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za Askari na mpaka sasa kuna nyumba za Askari ambazo zinaendelea kujengwa kwenye mikoa mbalimbali. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Venance Mwamoto na baada ya Bunge hili nilimwahidi nitakwenda Kilolo kwa ajili ya kujionea hali ilivyo. Ahsante

Name

Yussuf Salim Hussein

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chambani

Primary Question

MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:- Kuna baadhi ya Askari Polisi kupandishwa vyeo lakini hawapati stahili zao kama inavyotakiwa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari hao stahiki zao?

Supplementary Question 5

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri kwamba kuna Maaskari Polisi waliopandishwa vyeo, alipandishwa kutoka private kuja Koplo ametumikia Koplo kwa miaka minne, mpaka ameenda Sajenti hajapata mshahara ule wa Koplo na wengine mpaka wanafikia kustaafu wanakosa stahiki zao analipwa kwa mshahara ule aliotokea nao. Je, Mheshimiwa Waziri Askari kama hawa atawa-consider vipi katika zoezi analoendelea nalo ili wapate haki zao kulingana na Utumishi wao walivyotumikia nchi hii?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kusema kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, kwamba mishahara inaendelea kurekebishwa kwa Maofisa, Wakaguzi pamoja na Askari. Hata hivyo, kama kuna suala ambalo linamhusu Askari ambaye amemsema kwamba alipanda cheo na nirekebishe kidogo, Jeshi la Polisi hatuna private, tuna constable kuanzia constable akaenda Koplo, Sajenti na hajarekebishiwa, namwomba Mheshimiwa Yussuf anipe jina la Askari huyo ambaye amemsema ili nifuatilie nijue kwa nini apande vyeo vyote hivyo pasipo kurekebishiwa mshahara wake. Ahsante.