Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Alex Raphael Gashaza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwepo na tatizo kubwa la hali ya usalama katika Jimbo la Ngara tangu mwaka 1993 kutokana na kuwa mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi ambapo kuna mwingiliano mkubwa wa wageni/wahamiaji haramu kutoka nchi hizo. (a) Je, ni lini Serikali itaanzisha Kanda Maalum ya Kipolisi katika Wilaya ya Ngara ili kudhibiti hali ya usalama? (b) Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya polisi katika Kata ya Mabawe, Muganza, Kirushya, Mtobeye, Mbuba na Nyakisasa? (c) Kwa kuwa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara lina gari moja tu zima na lingine bovu bovu, je, ni lini Serikali itatupatia angalau magari mawili, moja kwa ajili ya Tarafa ya Rulenge na la pili kwa ajili ya Tarafa ya Murusagamba?

Supplementary Question 1

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nitaomba kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ngara kimejengwa tangu enzi za ukoloni na majengo yake yamechakaa pamoja na nyumba za watumishi kwa maana nyumba za askari wetu. Sasa ni lini Serikali itaweza kukarabati kituo hiki cha polisi na nyumba za askari wetu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, wananchi wa Jimbo la Ngara wameathirika kwa kiasi kikubwa sana na operesheni zinazoendelea hususani za Uhamiaji. Maeneo mengi Dar es Salaam, Kahama, Arusha, Ngara kwenyewe wananchi hawa wanapokamatwa kwa kuhisiwa na kueleza kwamba wanatokea Ngara moja kwa moja wanachukuliwa kwamba ni wahamiaji haramu. Wamekuwa wakipigwa na kuumizwa na baadaye baada ya kujiridhisha inaonekana kwamba ni Watanzania halisi. (Makofi)
Sasa je, Serikali iko tayari pale inapobainika kwamba wananchi hawa wamehisiwa, wakadhalilishwa, wakapigwa wako tayari kulipa fidia kwa hawa wananchi wanaokuwa wamedhalilishwa na kupigwa?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza alitaka kujua kuhusiana na uwezekano wa kukarabati Kituo cha Polisi Ngara pamoja na nyumba za polisi. Kama ambavyo nimejibu kwenye jibu langu la msingi kwamba dhamira hiyo kwa Serikali ipo na pale tu ambapo hali ya kifedha itaruhusu tutakarabati kituo hicho cha Ngara na nyumba za polisi pamoja na maeneo mengine nchini ambako kuna changamoto kubwa za uchakavu wa vituo na nyumba za polisi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na wananchi ambao wamepigwa na kuonekana kwamba wamedhaniwa kwamba si Watanzania. Kwanza si utaratibu wa Jeshi la Polisi kupiga raia ama hata wageni. Kuna utaratibu wa kisheria ambao ikiwa mgeni ama raia amevunja sheria unatakiwa uchukuliwe kwa mujibu wa sheria. Nadhani suala hili labda Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili tukae tuone jinsi gani tunaweza kulichunguza ili tujue hatua za kuchukuliwa baada ya hapo kama kutakuwa kuna ukiukwaji wa sheria, sheria iweze kufuata mkondo wake.

Name

Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwepo na tatizo kubwa la hali ya usalama katika Jimbo la Ngara tangu mwaka 1993 kutokana na kuwa mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi ambapo kuna mwingiliano mkubwa wa wageni/wahamiaji haramu kutoka nchi hizo. (a) Je, ni lini Serikali itaanzisha Kanda Maalum ya Kipolisi katika Wilaya ya Ngara ili kudhibiti hali ya usalama? (b) Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya polisi katika Kata ya Mabawe, Muganza, Kirushya, Mtobeye, Mbuba na Nyakisasa? (c) Kwa kuwa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara lina gari moja tu zima na lingine bovu bovu, je, ni lini Serikali itatupatia angalau magari mawili, moja kwa ajili ya Tarafa ya Rulenge na la pili kwa ajili ya Tarafa ya Murusagamba?

Supplementary Question 2

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Matatizo yaliyopo Ngara ni sawa kabisa tena yanapita ya Jimbo la Mlimba. Jimbo lenye kata 16 halina kituo cha polisi wala gari la polisi na kupelekea Mahabusu kukaa muda mrefu sana ili kuwapeleka katika Mahakama au Magereza yaliyoko kilometa 265. Je, ni lini sasa Serikali itaboresha miundombinu ya Jeshi la Polisi ndani ya Jimbo la Mlimba angalau uwapatie gari basi?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, ni sahihi katika Jimbo la Mlimba kuna upungufu ama ukosefu wa Kituo cha Polisi, lakini kama sehemu ya mkakati wa Serikali wa kujenga vituo 65 vya polisi nchi nzima tunaamini Mlimba ni moja ya katika maeneo hayo. Kwa hiyo, tu nimuombe Mheshimiwa Mbunge avute subira pale ambapo mpango huo utakapokuwa umekamilika kituo cha polisi kitapatikana Mlimba.

Name

Daniel Nicodemus Nsanzugwako

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Primary Question

MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwepo na tatizo kubwa la hali ya usalama katika Jimbo la Ngara tangu mwaka 1993 kutokana na kuwa mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi ambapo kuna mwingiliano mkubwa wa wageni/wahamiaji haramu kutoka nchi hizo. (a) Je, ni lini Serikali itaanzisha Kanda Maalum ya Kipolisi katika Wilaya ya Ngara ili kudhibiti hali ya usalama? (b) Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya polisi katika Kata ya Mabawe, Muganza, Kirushya, Mtobeye, Mbuba na Nyakisasa? (c) Kwa kuwa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara lina gari moja tu zima na lingine bovu bovu, je, ni lini Serikali itatupatia angalau magari mawili, moja kwa ajili ya Tarafa ya Rulenge na la pili kwa ajili ya Tarafa ya Murusagamba?

Supplementary Question 3

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Swali la kwanza la Mheshimiwa Gashaza lilikuwa ni Ngara kuanzishiwa Kanda Maalum ya Kipolisi na Wilaya ya Ngara, Kakonko, Kibondo, Kasulu na Kigoma ni maeneo ambayo yanapakana na nchi nne yaani Burundi, Rwanda, Congo na Zambia kwa upande wa majini Kusini. Ni kwanini Serikali isione umuhimu wa kuanzisha kanda maalum kwa sababu zone ile ndiyo zone inayopitisha silaha ambazo hatimaye zinakuja kutushambulia katikati ya nchi yetu. Ni kwa nini Serikali isione umuhimu wa wilaya hizo tano kuanzishiwa Kanda Maalum ya Kipolisi ili kudhibiti uingizaji wa silaha katika nchi yetu?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu katika swali langu la msingi kwamba kuna jitihada kadhaa ambazo tumezichukua za kuimarisha hali ya usalama katika maeneo ya Mkoa wa Kigoma kwa ujumla wake ikiwemo hasa maeneo ya Wilaya ya Ngara. Kutokana na jitihada hizo imepelekea kwamba eneo hilo kwa sasa hivi kukosa vigezo vya kuweza kuanzisha ama umuhimu wa kuanzisha Kanda Maalum. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge aridhike kwamba kwa sasa hivi akubaliane na sisi kwamba eneo la Ngara bado halijakidhi vigezo hivyo kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama katika maeneo hayo.