Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Ali Abdallah

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Tumbe

Primary Question

MHE. RASHID ALI ABDALLAH aliuliza:- Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kama vile LAPF, PSPF, PPF, NSSF na NHIF imesaidia sana kutoa mikopo hasa kwa Serikali kwa ajili ya maendeleo ya jamii:- Je, Serikali imefanya juhudi gani kurejesha mikopo hiyo kwa wakati?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili ni la muda mrefu sana kabla hata dhana ya kuunganisha Mifuko ilikuwa haijafikiwa, ndiyo linakuja leo. Pamoja na mambo hayo nitakuwa na swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, deni la trilioni 2.1 ndani yake kuna malimbikizo makubwa ya riba ambayo yamesababishwa na Serikali kwa kutokulipa kwa muda mrefu. Mifuko bado haijaunganishwa lakini riba haisubiri Mifuko kuunganishwa inaendelea. Ni hatua gani Serikali inachukua kuhakikisha kwamba Mifuko hii inaunganishwa haraka ili kunusuru riba hii isiongezeke? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba sheria tayari imeshasainiwa na Mheshimiwa Rais na kanuni zimeshakamilika. Ndani ya mwezi huu wa Tano Serikali inazipeleka kanuni kwa wadau ili tuweze kupata maoni yao na sisi kama Serikali tunatambua umuhimu wa kuiwezesha Mifuko kwa madeni yao haya, tuko tayari kulipa pale kanuni zitakapokuwa zimekamilika. Ahsante.