Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stanslaus Shingoma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nyamagana linalojengwa katika Kata ya Mkolani limechukua zaidi ya miaka minne sasa bila kukamilika:- (a) Je, Serikali haioni kuwa na miradi isiyokamilika kwa wakati kunarudisha nyuma maendeleo; (b) Je, ni lini sasa Serikali itapeleka fedha za kukamilsha jengo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Nataka kuuliza jambo moja kwamba majengo haya ya Serikali yanachukua muda mrefu kukamilika na matokeo yake yanagharimu fedha nyingi zaidi ambapo yangejengwa na kukamilika kwa wakati yangesaidia sana matumizi ya fedha za Serikali kutumika kwa uchache.
Mheshimiwa Spika, sasa pamoja na Serikali na jitihada zake kubwa, ni miaka 10 leo. Mwaka ujao wa fedha Mheshimiwa Waziri anatuahidi kwamba jengo hili litakamilika. Naomba sana tufanye jitihada hiyo ili fedha hizi ziletwe na jengo hili likamilike. Hii itachangia hata ukuaji wa uchumi kwenye lile eneo ambalo Jengo la Mkuu wa Wilaya limejengwa. Nakushukuru sana.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, napenda nimhakikishie Mheshimiwa Mabula na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, pamoja na mikoa yote na wilaya zote, tumepitisha hapa Bungeni shilingi bilioni 53 kwa ajili ya kujenga majengo ya Halmashauri na tumepitisha hapa shilingi bilioni 80 kwa ajili ya bajeti za maendeleo ya mikoa. Hizi fedha nataka niwahakikishie kwamba Serikali inaendelea kuwa stable kabisa katika masuala ya ukusanyaji wa fedha, fedha zitapelekwa, wala asiwe na wasiwasi wowote.