Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deogratias Francis Ngalawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA aliuliza:- Kumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa barabara pembezoni mwa Ziwa Nyasa, hususan Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Njombe; eneo hilo lenye urefu wa kilomita 150 hutegemea usafiri wa meli ambao hauna tija kwa wananchi walio wengi:- (a) Je, Serikali itawasaidia vipi wananchi wa maeneo hayo yenye vijiji 22 kupata barabara ya uhakika? maeneo hayo yenye vijiji 22 kupata barabara ya uhakika? (b) Kwa kuwa wananchi wameanza kutengeneza wenyewe barabara kwa nguvu zao. Je, Serikali inatoa tamko gani la kuunga mkono juhudi hizo za wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza, napenda kutumia fursa hii kuishukuru Serikali kwa kutupatia fedha hizo shilingi milioni 500 na ni kweli Mkandarasi G.S Contractor yupo site.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipokuwa nazungumza kwamba tuna baadhi ya vijiji wananchi wa Tanzania walioko kule hawajawahi kuona gari, baiskeli wala pikipiki, hiyo imeshuhudiwa hata na Naibu Waziri, Mheshimiwa Engineer Nditiye tulipokuwa naye kule. Je, baada ya kuwa tayari kipande hiki kidogo tumeshakipata, TARURA ina mpango gani sasa wa kuhakikisha inafanya kazi hiyo kwa haraka ili Vijiji vya Makonde, Kilondo, Nsele, Lumbila, Nkanda, Nsisi na Lifuma viweze kupata barabara? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu katika swali la msingi, kazi ambayo inaenda kufanyika ni kufanya usanifu kujua gharama ambazo zitatumika katika ujenzi wa barabara hii ni kiasi gani ili hatua ya pili iweze kufuata. Pia mimi mwenyewe nimepata fursa ya kutembelea Wilaya ya Ludewa, Jimboni kwa Mheshimiwa, kama kuna maeneo ambayo jiografia ni changamoto ni pamoja na eneo la Ludewa, ndiyo maana unaona kwamba kipande kidogo kinagharimu kiasi kikubwa cha fedha kama hivyo ambavyo nimetaja katika jibu langu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, maeneo ya Lupingo ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba yanafikika kwa njia ya barabara. Avute subira, nia ya Serikali ni njema yeye mwenyewe anashuhudia, naomba tuvumiliane hili litakamilika kwa wakati. (Makofi)

Name

Ajali Rashid Akibar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA aliuliza:- Kumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa barabara pembezoni mwa Ziwa Nyasa, hususan Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Njombe; eneo hilo lenye urefu wa kilomita 150 hutegemea usafiri wa meli ambao hauna tija kwa wananchi walio wengi:- (a) Je, Serikali itawasaidia vipi wananchi wa maeneo hayo yenye vijiji 22 kupata barabara ya uhakika? maeneo hayo yenye vijiji 22 kupata barabara ya uhakika? (b) Kwa kuwa wananchi wameanza kutengeneza wenyewe barabara kwa nguvu zao. Je, Serikali inatoa tamko gani la kuunga mkono juhudi hizo za wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ndogo ili niweze kuuliza swali ndogo la nyongeza. Matatizo ya meli pamoja na barabara yaliyopo Ludewa yanafanana sana na matatizo yaliyopo Mtwara, Lindi hadi Dar es Salaam. Shehena kubwa ya saruji kutoka Dangote huwa inasafirishwa kwa barabara hadi kufika Dar es Salaam, vilevile shehena kubwa ya mawe kutoka Kilwa huwa inasafirishwa hadi kufika Dar es Salaam kwa njia ya barabara, tatizo ambalo lingeweza kutatuliwa kwa kutengeneza zile meli za MS Mtwara pamoja na MV Lindi. Ni lini sasa Serikali itatengeneza meli zile za MS Mtwara na MV Lindi ili barabara ile kati ya Dar es Salaam hadi Mtwara isiharibike na shehena hiyo kubwa iweze kusafirishwa na meli hizo mbili? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba zile meli alizozizungumza Mheshimiwa Mbunge zina hitilafu, lakini tayari tumeshatuma mafundi na wataalam kwa ajili ya kwenda kuangalia gharama ambazo zinahusika kwa ajili ya matengenezo ya meli hizo. Kwa hiyo, tunamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati muafaka ukifika zitatengenezwa ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)