Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. EDWIN A. NGONYANI (K.n.y. MHE. ISSA A. MANGUNGU) aliuliza:- a) Je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza umeme kwenye maeneo ambayo hayamo katika miradi ya umeme vijijini, maeneo kama vile Changanyikeni, Ponde, Malela, Vikindu, Goroka A, B katika Kata ya Tuangoma na Majimatitu A, Vigozi, Machinjioni A, Mponda katika Kata ya Mianzini, Mzala, Kwa Mapunda, Kisewe, Dovya, Sai A, B katika Kata ya Chamazi? b) Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la low voltage katika Jimbo la Mbagala hasa maeneo ya Kiburugwa, Kilungule, Charambe, Kijichi, Kibondemaji Chemchem na Tuangoma?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Spika, pamoja na kusahisha jina la eneo la Kitungule badala ya Kitungule isomeke Kilungule.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Ali Mangungu anaishukuru sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa iliyoifanya katika kipindi hiki cha mwaka mmoja na kwa kweli wanaomba yale maeneo yaliyobakia yakamilishwe, kwa hiyo, eneo la kwanza ni ombi.
Mheshimiwa Spika, pili, ndugu zao wa Namtumbo wanaomba kuna vijiji 70 na miji midogo miwili. Katika miji midogo miwili mji mdogo mmoja tu mitaa yake ina umeme, vinginevyo vijiji vyote 70 pamoja na mitaa ya Mji Mdogo wa Lusewa havina umeme. Pamoja na kwamba dalili zinaonekana lakini muda unapita na hakuna dalili ya umeme kupatikana katika Wilaya hiyo nzima ya Namtumbo.
Ni lini Serikali itawasha umeme katika Wilaya ya Namtumbo?

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza tumepokea pongezi za Mheshimiwa Mbunge Mheshimiwa Issa Ali Mangungu na Serikali tunampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia maendeleo ya nishati katika Jimbo lake la Mbagala na ombi lake tumelipokea katika maeneo yaliyosalia kama nilivyosema mradi umekamilika kwa asilimia 90 basi asilimia 10 ndani ya muda mfupi itakamilika.
Swali lake la pili la ndugu wa kutoka Jimbo la Namtumbo. Kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema naomba nilitaarifu Bunge lako tukufu na niwapongeze Wabunge wote wa Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Njombe kwa kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa line ya kusafirisha umeme Makambako - Songea yenye urefu kilometa 250. Napenda nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge tarehe 01 na tarehe 02 tulifanya ziara kukagua mradi huo na kimsingi mradi umekamilika.
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa substation tatu Madaba, Songea - Makambako umekamilika, ujenzi wa line umekamilika, kinachoendelea sasa hivi ni usambazaji umeme katika maeneo ya vijiji 122, vijiji 60 ni Mkoa wa Ruvuma, na vilivyosalia ni Mkoa wa Njombe. Katika Jimbo lake la Namtumbo takribani vijiji 35 vitapata umeme kupitia mradi huu mkubwa wa ujenzi wa line ya Makambako - Songea.
Mheshimiwa Spika, naomba nilitaarifu Bunge lako mwezi huu Septemba tarehe 25 au 26 mradi huu utazindua rasmi na sasa hivi kinachoendelea ni test mbalimbali zinazoendelea katika line hii. Kuanzia tarehe 15 Septemba tutasafirisha umeme kwa mara ya kwanza kwenye Gridi ya Taifa kuelekea Songea Mkoa wa Ruvuma. Nawashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutuunga mkono na kwa kweli mambo mazuri. Ahsante sana.(Makofi)