Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Njalu Daudi Silanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itilima

Primary Question

MHE. NJALU D. SILANGA aliuliza:- Tanzania ni nchi yenye mazao ya biashara kama pamba, korosho, tumbaku na kahawa. Zao la pamba linazidi kuporomoka kutoka wastani wa ekari moja kilo 400 hadi kilo 120 kwa ekari moja ikilinganishwa na nchi kama China ekari moja kilo 2,000, India kilo 1,500, Burkina Faso kilo 1,200 na wastani wa uzalishaji wa dunia ni kilo 1,200 kwa ekari moja:- Je, Serikali ina mpango gani wa kunusuru zao hilo?

Supplementary Question 1

MHE. NJALU D. SILANGA: Mheshimiwa Spika, kwanza ahsante sana kwa kunialika kwenda kuona ngoma, niko tayari kwenda huko. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kwanza kumpongeza Naibu Waziri wa Kilimo kwa majibu yake mazuri aliyonijibu. Hivi sasa maeneo mengi yameonekana kuwa na ugonjwa wa mbegu hii UKM08. Je, Serikali inatoa tamko gani kwa wakulima wa zao la pamba kwa maeneo ambayo yanaathirika na ugonjwa huu Fusarium hasa ikizingatia kwamba viuatilifu vinavyokuja havifikii viwango na kusababisha mashamba mengi kuharibika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Naibu Waziri ameelezea kwamba kuna mkakati mzuri kwa mwaka 2016/2017 ekari moja imeweza kuzalisha kilo 300 lakini kwa mwaka 2016/2017 wastani ambao tumeweza kukusanya kwa nchi nzima kwa maana kwa mikoa 17 na wilaya 56 ni takribani kilo milioni 120. Kwa hiyo, atakubaliana nami kwamba zao la pamba linazidi kuporomoka. Ukigawanya kwa wastani katika zao zima kwa nchi nzima ni Mkoa mmoja tu wa Simiyu wenye kuzalisha kilo 70,000 na mikoa 16 ndiyo unaigawanya. Kwa hiyo, kama Wizara iko shughuli ya kufanya kuhakikisha zao hili linaongezeka kwa uzalishaji. Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, awali kabisa, naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu amekuwa akifuatilia sana juu ya zao zima la pamba na hasa ukizingatia na yeye pia ni mfanyabiashara wa zao hili la pamba.
Mheshimiwa Spika, nikija kwenye maswali yake mawili madogo ya nyongeza kwa ufupi kabisa na kwa pamoja ni kwamba zao la pamba kama zao la pamba na mbegu, sisi kwenye zao la pamba zile mbegu huwa inachukua muda mrefu sana na ukizingatia kwamba mbegu hizo tunazosema utafiti unafanyika muda mrefu muda wa karibu sana na kwa haraka ambao unaweza ukafanyika ni ile miaka mitano. Kwa maana hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote wajue kabisa kwamba suala zima la utafiti huwa linachukua muda mrefu na muda mfupi ambao unaweza ukafanyika ni kipindi cha miaka mitano.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake lile la pili la nyongeza kwamba kwa nini kilimo hiki cha zao la pamba kimeporomoka, ni kweli kwamba wakulima walikuwa hawafuati zile kanuni bora za kilimo cha pamba. Nichuke fursa hii kumpongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu amekuwa ni champion, amekuwa akihamasisha na akiwaeleza hata Wakuu wa Mikoa juu ya ufuatiliaji wa zao zima la pamba.
Mheshimiwa Spika, vilevile amemuagiza hata Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kuboresha suala zima la ugani. Pia kama Serikali tumejipanga kuhakikisha kwamba katika msimu wa 2018/2019, tutaboresha zao la pamba kutoka hiyo tani 300,000 kwa ekari hadi tani 600,000 kwa kuzingatia hayo maelezo ambayo nimesema ili wakulima wote nchini waweze kuhakikisha kwamba wanafuata kanuni bora za kilimo cha pamba. Mheshimiwa Spika, ahsante.