Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Othman Omar Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. OTHMAN OMAR HAJI aliuliza:- Pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuwa na uchakavu wa mitambo ya kuongezea ndege na miundombinu duni ya usafiri wa anga nchini, TCAA imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Shirika la Usafiri wa Anga Duniani kuanzia mwaka 2016 hadi 2019 na hivyo kuwa mwakilishi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Je, kupitia nafasi hii ya kipekee, Serikali kupitia TCAA ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya usafiri wa Anga hapa nchini, ili iweze kulingana na ile ya nchi nyingine za SADC?

Supplementary Question 1

MHE. OTHMAN OMAR HAJI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba katika majibu yake wajipange sana katika mikakati yao kwa sababu Shirika la Anga la Kenya bado wanatufilisi kwa kuchukua mapato ya nchi. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya mwaka 2015/2016 TCAA iliingia mkataba na Kampuni ya COMSOFT GMBH ya Ujerumani. Kwa kuweka mitambo ya kisasa ya kuongozea ndege na kufuatilia safari za ndege yenye thamani ya shilingi bilioni 3.4. Kwa sababu mkandarasi huyu hakuweka dhamana katika kazi, yake mnamo mwaka 2014/2015 mzabuni alitangaza kufilisika.
Kwa kuwa shirika liko kimya kuhusu suala hili Mheshimiwa Waziri naomba kukuuliza, ni kwa kiwango gani shirika limeweza kuokoa fedha hii ya walipa kodi zilizopotea? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali namba mbili, Mheshimiwa Waziri, Mamlaka ilipokutana na Kamati ya PIC ilikuwa na kilio kwamba wana ukosefu wa wataalam wenye sifa katika usafiri wa anga. Katika hotuba yako uliyoiwakilisha muda mchache tu mwaka huu ulisema kwamba Chuo cha Usafiri wa Anga Dar es Salaam kinatoa wataalam wa mafunzo tofauti na wenye viwango vya kimataifa wa ndani na nje ya Tanzania. Je, Mheshimiwa Waziri wataalam hawa…
...wataalam hawa wanaomaliza chuo unawapeleka wapi?

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Spika, kwanza nimuhakikishie tu kwamba kwa ufungaji wa rada nne hizo ambazo Mheshimiwa Rais amezindua tarehe 2 Aprili, tuna hakika anga letu lote tutalimiliki sisi kwa maana ya kuhakikisha usalama wake. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi kwamba nchi jirani zitafanya hicho kitu badala yetu. Lakini nikijibu swali lake la kwanza nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba fedha iliyolipwa na Serikali haijapotea bado ipo na sasa hivi kuna taratibu zinafanyika kuhakikisha kwamba pesa yetu inarudishwa kwa wananchi walipa kodi wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu ukosefu wa wataalam nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna wataalam 40 ambao wamepelekwa kusoma ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanaiendesha mitambo yetu hii ya rada ambayo inafungwa kwa ufanisi wa kutosha.