Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Tano imeusaidia sana Mji wa Songea kwa kuleta ndege za Bombadier ambazo zinatoa huduma zake katika Uwanja wa Ndege wa Songea. • Je, kwa nini uwanja huo hauongezwi urefu na kufanyiwa ukarabati ili kutoa huduma zaidi na kuruhusu ndege ziweze kutua kwa saa 24? • Je, kwa nini Serikali haiweki mashine za ukaguzi wa abiria (scanning machine) ili kuondoa adha kwa abiria kukaguliwa mizigo yao kwa kupekuliwa ambapo inadhalilisha na kupoteza muda?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake. Napenda kumuuliza swali la nyongeza kwamba wakati utaratibu wa kumpata Mkandarasi wa kutengeneza uwanja huo unaendelea, kwa nini huduma ya ndege isiendelee? Maana yake hivi sasa huduma ya ndege imesitishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa nini huduma za ndege katika Uwanja wa Songea ambazo zinawasaidia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Njombe zisiendelee wakati Mkandarasi anaendelea kutafutwa? (Makofi)

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tumesimamisha kwa muda huduma za usafiri wa ndege katika kiwanja hicho ili kupisha marekebisho yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunategemea kuongeza tabaka la lami, kwa sababu sasa hivi ndege ikitua na kuondoka inapeperusha changarawe ambapo tuna wasiwasi zinaweza zikaingia kwenye propeller zikahatarisha usalama wa abiria, lakini na ndege vilevile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunafanya ukarabati wa uwanja kwa kuondoa mashimo ambayo yako kwenye uwanja ule ili tuepushe ajali. Hata hivyo, tunahakikisha kwamba huduma zitarudi hivi karibuni baada ya kuwasiliana na TAA kwamba wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba hizo changamoto zilizoko katika uwanja huo zinarekebishwa.