Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. GIBSON B. OLE MEISEYEKI aliuliza:- Hivi karibuni Serikali ilianza zoezi la kubomoa nyumba kwenye vyanzo vya maji na waathirika wa operesheni hiyo sheria imewakuta na wengi wao walikuwa kwenye maeneo hayo tangu enzi za ukoloni hususani wananchi wa Kata ya Kiranyi:- Je, Serikali inawafikiriaje wananchi hawa ambao sheria imewakuta kwenye maeneo hayo?

Supplementary Question 1

MHE. GIBSON B. OLE MEISEYEKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nirekebishe jina langu tu naitwa Gibson Blasius Ole Meiseyeki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni kulikuwa na zoezi la ubomoaji uliofanyika katika shamba la Mheshimiwa Mbowe katika Wilaya ya Hai. Je, ofisi yako ilibariki tukio hili?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa, Arumeru Magharibi kuna mashamba mengi ya wawekezaji ambayo kiuhalisia yamejengwa kwenye maeneo ambayo pia ni vyanzo vya maji na wananchi wanakusudia kwenda kuisaidia Serikali kuondoa mashamba hayo ambayo kimsingi yanaharibu vyanzo vyetu vya maji. Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusiana na nia hii ya wananchi ya kuyaondoa mashamba yote ambayo yako kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kwa mujibu wa taratibu. (Makofi.) Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI naomba kujibu swali la ndugu yangu Gibson, naomba niishie hapo hapo huko mbele majina ya kimasai yasije yakanichanganya zaidi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama suala la kubariki zoezi lililofanyika Katamba katika shamba la Mheshimiwa Mbowe, kwa sababu hili jambo ni specific sana na sijajua harakati za pale, sitaki kulitolea comment katika hilo. Naomba nizungumze hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu wananchi wapo tayari sasa kushirikiana na Serikali, kuhakikisha kwamba inashirikiana vizuri kwenda kuondoa wale wananchi au mashamba yaliyopo katika eneo husika. Tukifanya rejea jana kulikuwa na mkutano mkubwa sana wa Waziri wa Mazingira na wadau kule katika Mkoa wa Iringa. Bahati nzuri niwashukuru baadhi ya Wabunge hasa katika Mkoa wa Iringa walikuwa katika mkutano ule, kuna mambo mahsusi yalijadiliwa katika suala la hivi vyanzo vya maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maelekezo yangu ni kwamba Wakurugenzi wote wameelekezwa utaratibu wa kufuata sasa katika vyanzo hivi vya maji. Imani yangu kubwa wazo hilo lake lililokuwa jema na kwa sababu tuna timu kule katika ngazi ya Mkoa na katika ngazi za Halmashauri, ukichukua na combination ya mawazo mazuri ya mkutano wa jana uliofanyika katika Mkoa wa Iringa, naamini litaenda kufanyika jambo sahihi kwa mujibu wa taratibu jinsi hali halisi ilivyo kule katika Mkoa wa Arusha hasa Arumeru.

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. GIBSON B. OLE MEISEYEKI aliuliza:- Hivi karibuni Serikali ilianza zoezi la kubomoa nyumba kwenye vyanzo vya maji na waathirika wa operesheni hiyo sheria imewakuta na wengi wao walikuwa kwenye maeneo hayo tangu enzi za ukoloni hususani wananchi wa Kata ya Kiranyi:- Je, Serikali inawafikiriaje wananchi hawa ambao sheria imewakuta kwenye maeneo hayo?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya sheria ya zamani ya mita 60 kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji, ilianza katikati ya mto mita 60 mpaka pembezoni mwa mto na mwaka jana tukairekebisha ikaanza mwisho wa mto na kuendelea, iliwaathiri wananchi wengi sana waliokuwa na mashamba ya asili wakati huo, ambao sasa hivi ndio wanakumbwa na hili tatizo la kuondolewa katika maeneo yao ya asili kama walivyofanya kwa Mheshimiwa Mbowe ambaye amekaa kwenye hilo shamba karibu miaka 80 iliyopita.
Je, Serikali imejipanga namna gani kufidia hawa wananchi kwa sababu marekebisho ya sheria ya mwaka jana yaliwakuta wananchi wakiwa wanaishi katika maeneo hayo? (Makofi)

Name

Julius Kalanga Laizer

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Monduli

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu katika utaratibu wa kisheria, mambo haya katika vyanzo hivi, maeneo chepechepe, maeneo oevu, yanakuwa defined katika mazingira mbalimbali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sababu kuna sheria ambayo imetungwa, kwa sababu tunajua kwamba kuna Waziri mwenye dhamana katika Ofisi ya Makamu wa Rais na bahati nzuri alipita mpaka Mkoa wa Arusha, Mkoa wa Kilimanjaro na Mikoa mingine, wakifanya ufafanuzi wa hizi sheria na utaratibu wake ukoje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu maamuzi yote yanaenda katika suala zima la mipango shirikishi, imani yangu kuwa ni kwamba, zoezi hili linapokwenda na ndio maana nirejee jibu langu la msingi, linapokwenda sasa kufanyika kubaini maeneo mbalimbali, kwamba hawa watu uhalisia wake ukoje, naamini maamuzi sahihi yatafanyika lakini baada ya kufanya jambo hili kuwa shirikishi zaidi kama tulivyoelekeza katika suala zima la Jimbo la Arumeru Magharibi.

Name

Ally Mohamed Keissy

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. GIBSON B. OLE MEISEYEKI aliuliza:- Hivi karibuni Serikali ilianza zoezi la kubomoa nyumba kwenye vyanzo vya maji na waathirika wa operesheni hiyo sheria imewakuta na wengi wao walikuwa kwenye maeneo hayo tangu enzi za ukoloni hususani wananchi wa Kata ya Kiranyi:- Je, Serikali inawafikiriaje wananchi hawa ambao sheria imewakuta kwenye maeneo hayo?

Supplementary Question 3

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria inasema mwambao wa Ziwa Tanganyika ni mita 60, lakini kuna upendeleo wa hali ya juu hasa kwenye Kijiji cha Kilando, wanavunjiwa watu na baadhi hawavunjiwi ambao wako chini ya hiyo kiwango cha mita 60. Je, Mheshimiwa Waziri anatoa tamko gani kuhusu wananchi wanaokaa mwambao mwa Ziwa Tanganyika kuacha upendeleo, kuvunjiwa baadhi ya watu na wengine kuachwa? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii sheria au utaratibu huu kwanza lengo lake kubwa ni kuhakisha tunalinda vyanzo vyetu vya maji. Leo hii katika nchi yetu maeneo mbalimbali, maeneo chepechepe, maeneo oevu, yote yanatoweka kwa sababu kuna uvamizi mkubwa sana na ndio maana tunakumbwa na janga kubwa na ukosefu wa maji katika maeneo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imani yangu kwamba, sheria itafuatwa hasa na Watendaji wetu wa chini, tusifanye double standard katika maeneo mbalimbali. Lazima kama tunafuata sheria utekelezaji wa sheria kwa sababu tunasema sheria ni msumeno, lazima ufuate hakuna kusema kumwonea mtu huyu na unamuacha mtu huyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Keissy kwamba wataalam wetu tutawaelekeza kwamba wanapokwenda kutekeleza sheria, lazima waache utaratibu wa double standard ili sheria itekelezwe kwa haki katika nchi yetu.

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. GIBSON B. OLE MEISEYEKI aliuliza:- Hivi karibuni Serikali ilianza zoezi la kubomoa nyumba kwenye vyanzo vya maji na waathirika wa operesheni hiyo sheria imewakuta na wengi wao walikuwa kwenye maeneo hayo tangu enzi za ukoloni hususani wananchi wa Kata ya Kiranyi:- Je, Serikali inawafikiriaje wananchi hawa ambao sheria imewakuta kwenye maeneo hayo?

Supplementary Question 4

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa kuwa lengo la Serikali ni kufanya vyanzo vya maji viendelee, lakini wanapowazuia wananchi kutolima kwenye vyanzo vya maji Serikali haiwapi mkakati wala kutengeneza eneo mbadala la kulima vyakula hivyo ikiwemo Mkoa wa Rukwa. Je, ni nini mkakati wa Serikali kabla haijawazuia kuwaandalia eneo mbadala la kuendelea na mazao hayo wanayolima? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli nafahamu, Mheshimiwa Aida ametoka Ziwa Rukwa, katika nchi yetu miongoni mwa Maziwa ambayo yapo hatarini kutoweka zaidi ni katika Ziwa letu Rukwa ambalo linaonekana sasa, wataalam wetu wanasema ukifanya tathmini miaka ishirini iliyopita na hivi sasa hali iko tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali jambo la kwanza ni kuhakikisha kwamba tunatoa elimu. Maana leo hii tunapozungumza wengine ndio wanaenda kuvamia vyanzo vya maji, kwa hiyo mkakati wa kwanza ni kutoa elimu. Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili tutawaelekeza wataalam wetu hasa jinsi gani wafanye, kuwabainisha wananchi waweze kutafuta fursa nzuri kwa sababu nchi yetu bado kuna maeneo na fursa kubwa katika suala zima la kilimo. Kwa hiyo jambo hili naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutalifanya, lakini kwanza ni elimu, watu wafahamu nini maana ya chanzo cha maji na nini athari yake chanzo cha maji kinapoharibika.