Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Silvestry Fransis Koka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Mjini

Primary Question

MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:- Serikali kwa nia njema ilirejesha sehemu ya shamba la Mitamba lililopo Kata ya Pangani, Kibaha Mjini kwa wananchi ambao walikuwa wanaishi katika maeneo hayo:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuendelea kurejesha maeneo mengine ya shamba hilo ambayo bado yanakaliwa na wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru na kumpongeza Waziri na Serikali kwa kuamua kurejesha takribani hekta 2963 kwa wananchi. Pamoja na kazi hiyo nzuri ya Serikali kwa wananchi ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika urejeshaji huo wa eneo hili kuna eneo dogo la takribani ekari 300 tu, ambalo lina zaidi ya kaya 250 ambalo halikufikiriwa katika mpango huu na ambapo limewafanya wananchi hawa wanaokaa katika eneo hili sasa wakae kwa mashaka na kujiona kwamba wao ni wanyonge kwa sababu hawakuwekwa katika mpango huu ambao uliwarejeshea maeneo wenzao.
Swali langu la kwanza, je, ni lini sasa Serikali itaamua kurejesha eneo hili dogo ili kuwatendea haki kama ilivyotenda haki kwa wananchi wengine na wananchi hawa wa Vingunguti waweze kujiona kwamba wametendewa haki kama hao wengine.
Swali la pili, kwa sababu Serikali imekuwa na nia njema na imechukua hatua mbalimbali, ni lini sasa Mheshimiwa Waziri pengine akishirikiana na Waziri wa Wizara ya Mifugo atatembelea eneo hili la Pangani maarufu linaitwa Vingunguti, ili tuweze sasa kukaa na wananchi na kupata ufumbuzi wa kudumu kutokana na mgogoro au tatizo hili la wakazi wa eneo hilo?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

himiwa Naibu Spika, naomba nikiri wazi tu kwamba Serikali haiwezi kuendelea kurudisha maeneo kwa wananchi, hasa katika hilo eneo ukizingatia kwamba eneo la awali lililokuwa na ukubwa wa hekta 4000 wananchi walipewa eneo la hekta 2963 sawa na asilimia 74 ya eneo lote. Hivyo kuendelea kulimega ni kufifisha pia azma ya Wizara ya Kilimo na Mifugo, katika kuendelea kuzalisha mitamba bora ambapo tunahitaji kuwapeleka wafugaji wetu katika maendeleo ya kuwa na ufugaji bora na endelevu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili niseme tu kwamba, Wizara imekuwa na nia ya dhati kufika katika lile eneo na kukutana na wananchi na hasa kukutanisha pande zote mbili, ukizingatia mara ya mwisho tumekuwepo kule tarehe 4/3/2016, lakini kama hiyo haikutosha Wizara yangu iko tayari kuendelea kukutana nao ili muafaka uweze kufikiwa.