Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Baadhi ya majengo na mabweni katika campus ya Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro yana uchakavu mkubwa sana ikiwemo miundombinu ya maji vyooni. Je, kuna utaratibu gani wa kuyafanyia ukarabati majengo haya na hasa kuwapunguzia shida wasichana wanaohitaji matumizi zaidi ya maji kuliko wengine?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa bado hali ya upatikanaji maji katika baadhi ya mabweni hasa vyooni haujarekebishwa pamoja na kutengewa hizo shilingi bilioni mbili na kupatikana hizo zilizopatikana. Je, ni lini Serikali itafanya zoezi la dharura kuhakikisha maji yanapatikana hasa hizi sehemu za vyooni wakati ukarabati mkubwa ukiendelea?
Swali la pili, nilitaka kufahamu katika ukarabati huo, je, Serikali ina huo mpango wa kuyabomoa kabisa yale majengo yaliyochoka na kuyaweka mengine yenye sifa na haiba ya Chuo hiki Kikuu cha Mzumbe na lini jambo hili litatekelezwa? Ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. la kwanza; katika kufanya marekebisho ya dharura tayari tumeshawaelekeza na hatua zinachukuliwa kuhakikisha kwa kutumia fedha zao za ndani Chuo cha Mzumbe kitaanza mara moja katika ukarabati wa miundombinu hiyo ya maji.
Lakini vilevile katika mpango wa kudumu kuhusiana pia na majengo ambayo yana hali mbaya, kwa mwaka huu wa fedha unaoanza Wizara yetu imejipanga vizuri sana na kwamba tuna fedha taslimu takribani shilingi bilioni 56 hizo tunazo mkononi kwa ajili ya kuboresha vyuo vyetu mbalimbali ikiwemo Mzumbe ambayo itapatiwa mabweni ya kutosha wanafunzi 3,000 pamoja na kumbi za mihadhara na majengo mengine ya utawala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vyuo vingine ni pamoja na Chuo Kikuu Huria ambacho kitapata jengo hapa Dodoma, Chuo cha Ushirika-Moshi lakini pia mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pale DUCE.

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Baadhi ya majengo na mabweni katika campus ya Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro yana uchakavu mkubwa sana ikiwemo miundombinu ya maji vyooni. Je, kuna utaratibu gani wa kuyafanyia ukarabati majengo haya na hasa kuwapunguzia shida wasichana wanaohitaji matumizi zaidi ya maji kuliko wengine?

Supplementary Question 2

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona.
Wakati Serikali inajibu swali mwezi Januari mwaka huu iliahidi kutenga fedha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya ukarabati na kuvifufua vyuo vya watu wenye ulemevu; na kwa kuwa fedha hii haijatengwa, je, Serikali ina kauli gani kwa hili? Ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Wizara inazo fedha kwa ajili ya kufufua baadhi ya vyuo vya watu wenye ulemavu kupitia mradi wake wa P4R. Kwa hiyo naomba uwe na amani ni kwamba zoezi hilo litafanyika kama ambavyo tumeanza katika shule nyingine ikiwemo shule ya Luwila pale Songea, shule ya Kipera pale Iringa na nyinginezo.