Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saumu Heri Sakala

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SAUMU H. SAKALA aliuliza:- Baadhi ya Waajiri ikiwemo Mashirika binafsi wamekuwa wakiwanyima haki ya msingi wafanyakazi wao kujiunga katika vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini kwa kutishia au kuwatafutia sababu ya kuwafukuza kazi pindi wanapojiunga na vyama hivyo:- a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka Sheria itakayowabana waajiri wenye tabia ya kuwatishia au kuwafukuza kazi pale wanapojiunga na Vyama vya Wafanyakazi nchini? b) Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa waajiri na kuwalazimisha kubandika Sheria hii ofisini kwa wafanyakazi ili wajue haki zao?

Supplementary Question 1

MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, sasa Waziri anaweza kukubaliana nami kwamba kuna uhaba mkubwa wa elimu juu ya suala la sheria hizi na kwamba muda umefika sasa Serikali iweze kutilia mkazo juu ya kutoa elimu hii kwa wafanyakazi pamoja na waajiri?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, mpaka sasa Serikali imekwishashughulikia waajiri wangapi ambao kwa namna moja au nyingine wamewabagua wafanyakazi ambao tayari wamejiunga katika Vyama vya Wafanyakazi?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la kwanza la elimu juu ya Sheria za Kazi, Wizara yetu imeendelea kutoa elimu hiyo kupitia Vyama vya Wafanyakazi, pia kupitia makongamano na warsha na semina mbalimbali, kuweza kuwaelimisha wafanyakazi, waajiri na umma kwa ujumla namna ambavyo sheria zetu zinaelekeza mambo gani yatiliwe mkazo. Hata hivyo, tunaendelea kutilia mkazo eneo hili na tutakuwa na vipindi tofauti kupitia katika redio na televisheni ili Umma wa Watanzania uweze kufahamu namna gani sheria hizi zinafanya kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nichukue wito huu kuwaomba wenzetu wa Vyama vya Wafanyakazi kwa kushirikiana na Wizara, tufanye kazi hii kwa pamoja ili tuweze kuwaelimisha waajiri na wafanyakazi sheria za kazi zinavyoelekeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika sehemu ya pili ya swali lake, amezungumzia kuhusu idadi ya waajiri wangapi tumekwishawashughulikia ambao wamewabagua wafanyakazi. Ofisi yetu kupitia Maafisa Kazi ambao wamekuwa wakifanya kaguzi mara kwa mara, wamekuwa wakipita maeneo tofauti kubaini matatizo haya na kuwachukulia hatua wale waajiri ambao wanashindwa kutii masharti ya sheria, hasa hii Sheria Na. 6 ya Mwaka 2004.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana ya idadi, nitamtafuta Mheshimiwa Mbunge nimpatie taarifa kamili ni kwa namna gani tumewashughulikia hao waajiri waliowabagua wafanyakazi wao specifically, lakini tumekuwa tukifanya kaguzi hizi na tunayo orodha ya waajiri wengi tu ambao wameshindwa ku-comply na orders zetu ambazo zimefanyika baada ya ukaguzi.