Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Raphael Michael Japhary

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL aliuliza:- Je, Serikali imejipanga vipi kumaliza madai ya msingi na ya muda mrefu kwa waongoza watalii, wapagazi na wapishi kutambuliwa kwa kima cha chini cha mishahara, mikataba ya kazi inayoendana na kazi zao, malipo ya posho kwa huduma wanazotoa kwa siku, sera shirikishi katika kutatua matatizo yao na utalii wa nchi kwa ujumla na malipo ya huduma za jamii kama vile afya na majanga?

Supplementary Question 1

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali kuhusu tatizo hilo, lakini bado tatizo hili ni kubwa na linaendelea. Mijadala juu ya wapagazi, waongoza watalii na wapishi imekuwa ya muda mrefu baina ya Serikali na waajiriwa hawa, lakini utekelezaji wa makubaliano umekuwa hafifu sana.
Swali la kwanza, je, Serikali haioni kwamba kuna haja kwa sasa kwenda kuonana na waajiriwa kuongea nao ana kwa ana, kujua ni kwa kiwango gani miongozo hii ambayo wameipeleka imetekelezwa na imekuwa na tija kwa hao watu ambao ndio waathirika wa tatizo hili?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na utaratibu kwamba wanaoshughulikia matatizo ya watalii imekuwa ni kampuni ya nje na sio watu wa ndani. Ni kwa nini Serikali haioni haja ya kushirikisha kampuni za ndani kuhakikisha kwamba inasimamia suala la porters na waongoza watalii na inaliacha katika kampuni za nje? Ahsante sana.(Makofi)

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tunakubaliana kabisa kwamba kuna haja ya kuonana na waajiriwa ili kuweza kubaini kama kweli yale makubaliano tuliyoyafikia pale Arusha yametekelezeka. Na mimi naomba kumwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya kikao hiki cha Bunge tutapanga safari ya kwenda kuonana na wale ili tuweze kuangalia utekelezaji wa hayo mambo yote.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kuhusu matatizo ya hawa wapagazi kwamba yanatatuliwa na kampuni ya nje, hili ni suala ambalo nimelisia sasa hivi, lakini nadhani tutalichukulia hatua na tutahakikisha kwamba matatizo ya Watanzania yanashughulikiwa na Watanzania wenyewe kupitia mifumo iliyowekwa na makampuni yetu yako tayari kabisa kushughulikia hili tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge, hili tutalishughulikia na kulifanyia kazi.