Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Martin Alexander Mtonda Msuha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:- Kwa takwimu za miaka ya hivi karibuni uzalishaji wa kahawa Wilayani Mbinga umeonekana kushuka kwa mkulima mmoja mmoja (out growers). Na sababu mojawapo ya kushuka kwa uzalishaji huo ni kuzeeka kwa miti ya kahawa. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapelekea wakulima wa Mbinga mbegu mpya ili kuinua uzalishaji? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka mnada wa kahawa Wilayani Mbinga, badala ya minada hiyo kuendelea kufanyika Moshi? (c) Je, Serikali ina mkakati gani wa kupiga marufuku kabisa uuzaji wa kahawa mbichi ikiwa shambani, maarufu kama “magoma” Wilayani Mbinga?

Supplementary Question 1

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, jambo mojawapo linaloyumbisha uzalishaji wa kahawa hususan Mbinga, ni kutokuwa na bei ya uhakika mwaka hadi mwaka. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuanzisha mfuko wa kuimarisha bei ya mazao hususan kahawa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kuambatana na mimi baada ya mkutano huu, ili akajionee mwenyewe ni jinsi gani utekelezaji na uzambazaji wa miche mipya ya kahawa unavyofanyika na Kituo cha TaCRI - Ugano, kama ilivyojibiwa kwenye swali la msingi? Ahsante sana.

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge wa jimbo hilo kwa ajinsi ambavyo anafuatilia kwa ukaribu sana katika zao zima hili la kahawa katika Jimbo lake. Lakini nikija katika swali lake la (a) ni kwamba, sisi kama Wizara kupitia Bodi ya Kahawa tunatoa bei elekezi kwa wakulima wale wadogowadogo wote kwa maana ya kwamba, farm gate market kwamba wawe wanapata bei elekezi kupitia njia ya mtandao wa simu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile tumegundua kwamba, njia hii ya mtandao wa simu iko more effective ukilinganisha na ile minada mingine, lakini hii tunaifanya kila wiki. Lingine naomba nitoe rai hata kwa wakulima wale wadogowadogo wote katika mashamba kwamba, wanapaswa wazingatie sana ubora wa zao hili la kahawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine vilevile kule Moshi ambako tunafanya mnada, huu mnada kule Moshi hatuwezi tukafanya kwa bei elekezi kwa sababu, mnada wa kule unategemea sana soko la dunia na kwa maana hiyo, soko la dunia inategemea na wakati wa ile market price iliyoko wakati huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho naomba nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba niko tayari kuongozananae kwenda kujithibitishia zao la kahawa. Ahsante.