Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Richard Mganga Ndassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Serikali imekamilisha mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Mji wa Ngudu na vijiji vilivyo karibu na mji huo Wilayani Kwimba. Mradi huo unatoa maji ya uhakika kuliko miradi ya visima vifupi ambavyo ni vya msimu. Lakini Mji Mdogo wa Malampaka na vijiji vingine vya karibu kama Jihu, Bukigi, Muhida, Lali, Nyabubinza na Mwang’honoli ambavyo vipo karibu na Mji wa Ngudu havijaunganishwa kwenye mradi huo. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha Mji Mdogo wa Malampaka na vijiji vya Jihu, Bukigi, Muhida, Lali, Nyabubinza na Mwang’honoli katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwapatia wananchi maji ya uhakika?

Supplementary Question 1

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali ilitenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya Mradi wa Maji Sumve, Madya na Malampaka, mwaka 2017/2018 ilitenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya mradi huo. Sasa Mheshimiwa Waziri katika majibu yake, kwa sababu ili maji yafike Mji wa Malampaka ni lazima yafike Sumve na Malya. Sasa nataka kujua, tulitegemea kwamba ungetaja, angalau kwamba Serikali imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya mradi huo, lakini hukutaja hata kidogo. Sasa swali Mheshimiwa Waziri, pesa zilizotengwa sasa hivi hazipo tena au mradi huo umeshakufa?

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, majibu niliyoyatoa haya yanalingana na swali lilivyoulizwa na Mheshimiwa Mashimba. Lakini kwa maana ya kutaka afahamu mradi wa kupeleka maji Sumve mpaka Malampaka, tumetenga fedha hizo, mwaka huu, shilingi bilioni mbili, kwanza kwa ajili ya kukamilisha usanifu na makabrasha ya zabuni ili kusudi tuweze kutangaza tender ya kupeleka maji Sumve mpaka Malampaka. Nia ya Serikali ipo palepale, hakuna mabadiliko, hata kama tungesema tu hapa bila utekelezaji ingekuwa haitusaidii, lakini nia ya Serikali ipo na lazima tupeleke maji Sumve, Malya na Malampaka.

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Primary Question

MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Serikali imekamilisha mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Mji wa Ngudu na vijiji vilivyo karibu na mji huo Wilayani Kwimba. Mradi huo unatoa maji ya uhakika kuliko miradi ya visima vifupi ambavyo ni vya msimu. Lakini Mji Mdogo wa Malampaka na vijiji vingine vya karibu kama Jihu, Bukigi, Muhida, Lali, Nyabubinza na Mwang’honoli ambavyo vipo karibu na Mji wa Ngudu havijaunganishwa kwenye mradi huo. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha Mji Mdogo wa Malampaka na vijiji vya Jihu, Bukigi, Muhida, Lali, Nyabubinza na Mwang’honoli katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwapatia wananchi maji ya uhakika?

Supplementary Question 2

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Ninapenda kujua kwamba Maswa tumekuwa na tatizo kubwa sana la maji, kwa kweli hali ni mbaya na inahitajika hali ya dharura kutatua tatizo la maji katika Mji wa Maswa na maeneo yake. Sasa ninaomba Mheshimiwa Waziri atusaidie, anatuhakikishia vipi kwamba kuna njia mbadala ya kupata maji katika Mji wa Maswa kwa sababu bwawa tunalolitumia limekauka kabisa? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza, nikiri, ni kweli bwawa ambalo Mji wa Maswa ulikuwa unategemea limekauka, na hii inatokana na matumizi yasiyokuwa endelevu ya wafugaji ambao walikuwa wanafuga jirani na lile bwawa kuweza kuzalisha matope na hivyo kufanya lile bwawa kujaa matope na maji kukauka. Kwa hiyo, Serikali tumetenga bilioni 1.1 katika Halmashauri ya Maswa, sasa katika fedha zile wanaweza wakatumia sehemu ya fedha hiyo katika kutafuta mpango wa dharura ili kuhakikisha kwamba wananchi wa pale wanapata maji.
Mheshimiwa Spika, lakini kwa ujumla, Mkoa wa Simiyu, tunao mpango mkubwa wa kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Bariadi na wilaya hizo zote ambao unafadhiliwa na KfW pamoja na Global Climate Fund, huu ni Mfuko wa Mazingira Duniani, kwahiyo fedha hizo, Euro milioni 100 na Euro milioni 25 tayari tumezipata. Sasa hivi tunakamilisha tu usanifu wa kina na muda si mrefu tutatangaza tenda ili tuweze kuujenga mradi ule, huo ndio utakuwa jibu la Mkoa huu wa Simiyu kuliko hivi visima ambavyo kwa muda mfupi vinakuwa vinakauka.