Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Wilaya ya Urambo inapokea umeme kutoka kwenye kituo cha kupoozea umeme cha Kaloleni umbali wa kilometa 90 kufika Urambo ambako ndiko kiliko kikata umeme inapokuwa kumetokea tatizo katika njia. Aidha, chanzo hicho cha umeme pia kimetegemewa na Wilaya ya Kaliua, Jimbo la Ulyankulu na vijiji vya Ikomwa, Igange, Tumbi, Ilolangulu hadi Ugoola (Tabora na Uyui); uzoefu unaonyesha kwamba kama kukitokea tatizo la kiufundi katika njia huwa inasababisha kukatika kwa umeme katika njia nzima likiwemo Jimbo la Urambo na kusababisha malalamiko mengi kwa TANESCO. Je, kwa nini Serikali isijenge kituo cha kupoozea umeme (substation) karibu na Wilaya ya Urambo ili kiweze kutoa umeme wa uhakika katika Wilaya hiyo inayozidi kukua katika mahitaji ya umeme hasa katika kutekeleza sera ya viwanda na katika taasisi zinazotoa huduma za kijamii kama hospitali, shule na kadhalika kwenye Jimbo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, awali ya yote nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jibu zuri pamoja na Serikali kwa ujumla kwa kukubali ombi letu la wananchi wa Urambo la kujenga kituo cha kupoza umeme (substation) Wilayani kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la nyongeza linasema, je, Serikali inaweza kuwahakikishia wananchi wa Urambo kwamba katika Awamu ya Tatu ya REA vijiji vyote vya Wilaya ya Urambo vitapata umeme? (Makofi)

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, napenda kumpngeza Mheshimiwa Margaret Sitta kwa juhudi kubwa anazofanya kufuatilia maendeleo ya wananchi wa Urambo, hongera sana Mheshimiwa Sitta. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini niseme tu kwamba ni kweli
vijiji vyote 27 vilivyobaki katika Jimbo la Urambo vitapata umeme ikiwemo Yerayera, Igembesabo, Ifuta na vijiji vingine. (Makofi)