Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Susanne Peter Maselle

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELE aliuliza:- Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuja na mikakati yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakiki watumishi wa umma, zoezi ambalo halikuwekewa muda wa kuanza na kumaliza (time frame) hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa na hata kuharibu mfumo wa watumishi wa umma, ikiwemo namna ya kuajiri. (a) Je, Serikali inatoa kauli gani kwa watumishi wa umma walioajiriwa na kusainishwa mikataba ya ajira ndani ya Serikali ambapo ghafla mwaka 2016 Rais alitoa kauli ya kusimamisha ajira kupisha ukaguzi wa watumishi hewa? (b) Je, Serikali inatambua kuwa watu hao tayari walikuwa watumishi na mchakato wa kuwaingiza kwenye payroll ulishaanza, lakini ukasitishwa ghafla na sasa wako mtaani na hawajui hatma yao?

Supplementary Question 1

MHE. SUSANNE P. MASELE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Ni lini sasa Serikali itaondoa hii dhana ambayo imeanza kujengeka kwamba Serikali haiwezi kuajiri kwa sababu haina fedha na kwamba Mheshimiwa Rais ndiye amekuwa akiajiri kwa utashi wake bila kufuata sheria?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali inajigamba kwamba imekusanya mapato mengi na imeondoa Wafanyakazi hewa, lakini ni kwa nini haijapandisha mshahara wala kupandisha watu madaraja? Serikali iwaambie Watumishi, ni kwanini haifanyi hivyo? (Makofi)

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza kabisa napenda kusema hakuna dhana kwamba Serikali haina uwezo wa kuajri. Wote mnafahamu katika mwaka wa 2015/2016 mazoezi yaliyokuwa yakiendelea katika uhakiki, lengo letu kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na idadi ya rasilimali watu ambayo tuna uhakika nayo, pia kujiriddhisha fedha ambayo tunalipa kama kweli ni thamani ya fedha kulingana na rasilimali ambayo ipo kazini.
Mheshimiwa Spika, tunashukuru kwa kufanya hivyo, tumeweza kuondoa zaidi ya watumishi hewa 19,708 ambao endapo wangeendelea kubaki katika orodha ya malipo ya mshahara, wangeisababishia Serikali hasara kila mwezi ya zaidi ya shilingi bilioni 19.8 fedha ambazo zingeweza kwenda kutumika katika miradi mingine ya maendeleo ya nchi.
Mheshimiwa Spika, ukiangalia tu katika mwaka huu wa fedha, tayari katika bajeti yetu tuliji-commit kama Serikali kwamba tutatoa ajira katika mwaka huu wa fedha 2017/ 2018 zaidi ya ajira 52,436. Pia tumeshaanza, ukiangalia katika mwaka huu wa fedha ambao tulikuwa tunaumalizia mpaka Julai, tayari tumeshatoa zaidi ya vibali vya ajira 10,184 na zaidi ya vibali vingine 4,816 pia viko katika taratibu za kutolewa kwa ajili ya kuziba mapengo yaliyojitokeza kutokana na suala zima la vyeti vya kughushi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala zima la kupandisha mishahara pamoja na vyeo au madaraja; katika suala la mishahara, mwaka huu kilichofanyika na nimekuwa nikilisema mara nyingi, ni kweli hatujapandisha mishahara. Hatujapandisha mishahara kwa sababu bado tunaendelea kuangalia hali ilivyo, pia na hali ya kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, tulichokifanya kwa mwaka huu ni nyongeza ya miashahara ya mwaka ambayo ni annual increment na wakati wowote kuanzia sasa nyongeza hiyo ya mishahara ya mwaka itaanza kutekelezwa.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa madaraja, tayari fedha ilishatengwa. Kuna zaidi ya shilingi bilioni 660 zimeongezeka katika bajeti ya mwaka huu ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2016 iliyokuwa shilingi trilioni 6.6. Mwaka huu tumetenga zaidi ya shilingi trilioni 7.205 na hii itasaidia kulipa maadeni ya watumishi, itasaidia pia kupandisha watumishi zaidi ya 193,166 na tunaamini wakati wowote stahiki hizo watumishi wataweza kuzipata.
Mheshimiwa Spika, hayo ndiyo maelezo ya Serikali na hakuna dhana iliyojengeka kwamba hatuwezi kuajiri wala kupandisha mishahara. (Makofi)

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELE aliuliza:- Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuja na mikakati yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakiki watumishi wa umma, zoezi ambalo halikuwekewa muda wa kuanza na kumaliza (time frame) hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa na hata kuharibu mfumo wa watumishi wa umma, ikiwemo namna ya kuajiri. (a) Je, Serikali inatoa kauli gani kwa watumishi wa umma walioajiriwa na kusainishwa mikataba ya ajira ndani ya Serikali ambapo ghafla mwaka 2016 Rais alitoa kauli ya kusimamisha ajira kupisha ukaguzi wa watumishi hewa? (b) Je, Serikali inatambua kuwa watu hao tayari walikuwa watumishi na mchakato wa kuwaingiza kwenye payroll ulishaanza, lakini ukasitishwa ghafla na sasa wako mtaani na hawajui hatma yao?

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Mheshimiwa Waziri ametueleza kwamba waliondoa watumishi hewa 19,708. Ni dhahiri kwamba kuondolewa kwa wafanyakazi wenye vyeti fake kumeathiri zaidi maeneo ya elimu na afya. Napenda kujua statistically ni vipi Serikali, maana yake ametuambia wataajiri; mpaka sasa hivi Serikali imeajiri walimu wangapi na wafanyakazi wa sekta ya afya? Maana yake kuna zahanati nyingine hazina kabisa watumishi.
Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine unakuta shule zina walimu watatu tu, tunaweza kuona ni madhara gani watoto wetu watapata. Sasa kama walikuwa na hili zoezi la vyeti fake, walijiandaa vipi ku-replace hawa wafanyakazi kwenye sekta ya elimu na afya? Ahsante.

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza kabisa kama nilivyoeleza, tumeshatoa vibali hivyo 10,184 na sasa hivi kwa upande wa elimu, tayari Wizara ya Elimu imeanza zoezi la kuchambua, wanatuma vyeti wale ambao walikuwa ni wahitimu na wanaostahiki kuingia, baada ya hapo watahakikiwa na kuweza kuingia katika ajira.
Mheshimiwa Spika, ukiangalia katika walimu kwa ujumla wake, katika ku-replace watumishi ambao wameondoka kwa walimu, ni zaidi ya walimu 3,012 wataweza kuajiriwa katika zoezi hili. Pia katika suala zima la sekta ya afya, tutaajiri zaidi ya watumishi 3,152. Hili ni katika kuziba pengo la walioghushi vyeti feki. Baada ya hapo, katika mwaka wa fedha 2017/2018 ajira bado ziko pale pale 52,436 na ni kutokana na hali ya uwezo wa kibajeti.