Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA aliuliza:- Kwa muda mrefu miembe imeendelea kushambuliwa na nzi na kuoza, minazi nayo hushambuliwa na ugonjwa wa kukauka na migomba hushambuliwa na ugonjwa wa mnyauko:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondokana na magonjwa hayo ili wananchi wazidi kufaidika na matunda ya mazao yao?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kwanza kwa majibu mazuri ya Serikali, hata hivyo lakini nina maswali mawili mafupi. Swali la kwanza, kuwa wakulima wengi sasa hivi wamechangamkia kilimo cha miembe na kwa kuwa Serikali imetoa mwongozo wa mafunzo kwa Maafisa Kilimo 117 tu; na kwa kuwa ni vikundi 19 tu vimepewa mafunzo; je, Serikali haioni haja kuweka mpango wa kutoa mafunzo zaidi ya maafisa kilimo ili kuweza kueneza kilimo hiki cha miembe ambacho kimechangamkiwa sana na wananchi sasa hivi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali imekiri kuwa imeanza utafiti, naipa pongezi na kwa kuwa mpaka sasa hivi Serikali imetoa starter kit kwa kikundi cha wakulima ambacho kinalima maembe tu. Hiki kikundi cha wakulima sana kimejikita Mkoa wa Pwani ambapo Mikoa ya Morogoro, Tanga mpaka Zanzibar, Tabora wanalima maembe na kwa kuwa ni lita 560 tu za kivutia wadudu zimetolewa tu. Je Serikali haioni kuwa kuna umuhimu wa kutoa starter kit angalau moja kwa mikoa hii inayolima miembe na kuongeza hii dawa ya kivutia wadudu kwa mikoa hii ili wakulima waweze kuendelea na kilimo hiki cha miembe?
Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia nawapa hongera sana vijana wangu wa SUA na wajasiriamali na Chuo cha SUA ambao wanaeneza miche ya miembe, hongereni sana.

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, kwanza nakubaliana nae kwamba mafunzo zaidi kwa Maafisa Kilimo yanahitajika na kwa fursa hii namwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Engineer Mtigumwe aandae mafunzo zaidi na hasa kwa maeneo yaliyotajwa ambayo yanazalisha maembe zaidi.
Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu kugawa starter kit na dawa hii ya eugenol ya kivutia wadudu nayo nakubaliana nayo tutaangalia uwezekano wa kupata fedha zaidi ya kuweza kueneza hizi starter kit kwa vikundi vya wakulima zaidi ya hicho kikundi kimoja kilichopata.