Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omary Tebweta Mgumba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Primary Question

MHE. OMARY T. MGUMBA aliuliza:- Kuna vyanzo vingine mbadala ya maji katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kama vile Mto Mbezi, Mto Ruvu na chanzo cha maji katika Kijiji cha Bamba Kiloka. Je, Serikali ina mpango gani wa muda mfupi, kati na muda mrefu wa kutatua changamoto ya maji safi na salama katika vijiji vya Mkuyuni, Madam, Luholole, Kibuko, Mwalazi, Kibuko na Mfumbwe katika kupanua na kuongeza uwezo wa tanki la Mto Mbezi ili liweze kukidhi mahitaji ya sasa?

Supplementary Question 1

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serilkali kupitia Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali imetenga shilingi milioni 368.5 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji katika vijiji vya Mkuyuni na Madam. Na kwa kuwa mwaka wa fedha 2016/2017 umebaki mwezi mmoja tu kumalizika, lakini mpaka sasa pesa hizi hazijafika; na kwa kuwa bajeti ya maji kwa ajili ya Morogoro imepunguzwa kutoka shilingi bilioni 4.2 ya mwaka jana mwaka huu imekuwa ni shilingi bilioni 1.5.
Je, Serikali inanipa commitment gani ya kuleta hela hizi shilingi milioni 368.5 kabla ya mwaka wa fedha uliobaki mwezi mmoja kuisha?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa katika mpango wa muda wa kati, Serikali imetenga shilingi milioni 150 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kupeleka maji katika Vijiji vya Lolole, Madam, Mwalazi, Kibuko na kitongoji cha Misala katika Kijiji cha Mkuyuni. Na kwa kuwa huu mradi wenyewe kwamba…
MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuna mradi wa maji katika kijiji cha Kibwaya ambao unakamilika muda si mrefu, je, Serikali badala ya kutafuta chanzo kingine cha maji, kwa nini isiongeze pesa katika mradi huu ili kupeleka maji katika vijiji hivi ambavyo nimevitaja vya Lolole, Misala, Madam na Kibuko?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli, mwaka huu wa fedha tulionao tulitenga zaidi ya shilingi bilioni 4 na kwamba mwaka unaokuja fedha hiyo imepungau kidogo. Lakini ni kwamba hivi sasa tunavyoongea tayari tumempatia shilingi milioni 976 na kwamba fedha hivyo wiki ijayo itatumwa kwa ajili ya kwenda kuendelea na utekelezaji wa miradi. Kutenga fedha kidogo ni kwa sababu wakati tunatenga shilingi bilioni nne kulikuwa na miradi inayoendelea na baadhi imekamilika. Ndio maana mwaka huu tumepunguza kidogo kwa sababu ya miradi iliyopo sasa ambayo imeelekea kukamilika haitakuwa na thamani kubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika, lakini pili kuhusu usanifu, tumetenga fedha kwa ajili ya usanifu wa miradi katika kijiji ambacho kinahitaji kupata maji, ameshauri kwamba tutumie chanzo kilichopo, tunaweka consultant, consultant ndiye atakayebainisha kama tutumie chanzo hicho au kingine kitakachokuwa kimepatikana.
Kwa hiyo, nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inafanyia kazi kuhakikisha maeneo yake yote yanapata maji safi na salama. Na bahati nzuri nilishatembelea kwake na tulienda kuzindua miradi ambayo tayari mingine imeshakamilika. Utekelezaji utaendelea na katika Jimbo lake Fulwe itapata maji ya kutoka Chalinze mara baada ya mradi wa Chalinze kukamilika.