Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Hospitali ya Vwawa Wilayani Mbozi inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitanda vya kulalia wajawazito pamoja na vile vya kujifungulia, pia wodi ya akinamama ni ndogo huku ukizingatia kuwa hospitali hiyo inahudumia Wilaya ya Mbozi na Momba:- Je, ni lini Serikali itajenga wodi ya akinamama kubwa yenye vifaa vya kutosha ili wanawake hawa waondokane na adha ya kulala wawili wawili?

Supplementary Question 1

MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Waziri japokuwa niseme kwamba majibu haya hayaridhishi na wala hayajatosha.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la msingi nilitaka kujua kwamba Serikali ina mpango gani wa kujenga wodi mpya ya akinamama katika Hospitali hii ya Wilaya ya Mbozi ukizingatia kwamba hospitali hii inahudumia wilaya mbili mpaka sasa. Hali halisi ilivyo pale kuna vitanda 25 tu vya akinamama vya kulala baada ya kujifungua lakini kwa siku wanawake wanaozalishwa katika hospitali hiyo ni wanawake 42 mpaka 50. Kwa hiyo, kukarabati hili jengo hakuwezi kusaidia. Kwa hiyo, swali langu la msingi nataka kujua kwamba Serikali ina mpango gani wa kujenga wodi ya akinamama mpya na kubwa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, katika
swali langu la msingi pia nataka kujua kwamba Serikali ina mpango gani wa kujenga Hospitali ya Wilaya ya Momba?Hili jambo nimekuwa nikilipigia kelele sana katika Bunge hili kwamba mpaka sasa Wilaya ya Momba hawana Hospitali ya Wilaya. Hali hiyo inapelekea usumbufu sana kwa sababu mara nyingi wanalazimika kuja kutibiwa katika hospitali ya Mbozi ambayo pia nayo jengo lake ni dogo. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Naibu Waziri aniambie ni lini sasa Serikali itajenga Hospitali ya Wilaya ya Momba? Ahsante.(Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge, haya yote yanatokana na needs za Wabunge wenyewe tunavyokaa katika vikao vyetu. Kwenye vikao vyetu ndipo ambapo tunaweka priority nini kifanyike. Eneo hili priority ya kwanza imeonekana ni lazima tutenge shilingi milioni 180 kwa ajili ya kufanya ukarabati huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba niseme mipango hii yote inaanzia kwetu sisi Wabunge katika maeneo yetu tunapofanya needs assessment au tunapopanga mipango yetu. Hata hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Juliana kwa jinsi anavyopigania haki za akinamama na watoto Serikali tutafanya kila liwezekanalo kuona jinsi gani tutafanya kwa sababu pale Vwawa sasa hivi ndiyo kama Makao Makuu. Licha ya ukarabati huu, lakini tutaangalia nini kingine kifanyike lengo kubwa ni akinamama na watoto hasa wanaozaliwa waweze kuwa katika mazingira salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Hospitali ya Momba, niliongea na Mkuu wa Mkoa wetu wa Songwe, Mama Chiku Gallawa wakati tunafanya mikakati ya ukarabati wa vituo vya afya 100, hili jambo aliweka kama priority na aka-identify kwamba Momba haina Hospitali ya Wilaya. Tulibadilishana mawazo tukaona lile eneo la awali ambalo limepangwa kuwa Makao Makuu ya Halmashauri ya Momba kile kituo cha afya cha pale tukiwekee miundombinu ya kutosha ili wananchi wa eneo lile waweze kupata huduma ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Juliana kwamba tutafanya kila liwezekanalo kuhusiana na hoja hii na kwamba katika Makao Makuu ya Momba tunaenda kufanya uwekezaji mkubwa sana ndani ya kipindi hiki hiki kabla ya mwezi wa saba. Kilio cha wananchi wa pale ni kwamba wanapata shida na Serikali tumesikia kilio hiki, tutaenda kufanya kazi kubwa na ya kutosha kuwasaidia akinamama na watoto wa maeneo yale. (Makofi)

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Hospitali ya Vwawa Wilayani Mbozi inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitanda vya kulalia wajawazito pamoja na vile vya kujifungulia, pia wodi ya akinamama ni ndogo huku ukizingatia kuwa hospitali hiyo inahudumia Wilaya ya Mbozi na Momba:- Je, ni lini Serikali itajenga wodi ya akinamama kubwa yenye vifaa vya kutosha ili wanawake hawa waondokane na adha ya kulala wawili wawili?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja la nyongeza. Matatizo yaliyopo Momba ni sawa kabisa na matatizo yaliyopo katika Mkoa wa Kigoma ikiwa ni katika Wilaya ya Kakonko na Buhigwe. Wilaya hizo ni mpya na zimekuwa zikipata huduma kutoka kwenye Wilaya Mama. Ni lini Wilaya ya Kakonko na Buhigwe zitapatiwa Hospitali ya Wilaya? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, anavyosema Mheshimiwa Mbunge Genzabuke ni kweli Kakonko wanatumia Kituo cha Afya cha pale Kakonko, hali kadhalika Buhigwe hawana Hospitali ya Wilaya. Kipindi kile nilivyofika Kakonko na Buhigwe tulifanya makubaliano fulani juu ya nini kifanyike kama mipango ya awali kurekebisha hali hii.
Mheshimiwa Naibu Spika,pale Buhigwe kwanza tunaenda kufanya ukarabati mkubwa wa Kituo cha Afya cha Buhigwe kwa kukipatia wodi ya upasuaji na wodi kubwa ya wazazi na vifaa vyote vinavyowezekana. Jambo hili tunalipanga kama Mungu akijalia kabla ya mwezi Agosti tutakuwa tumelitekeleza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutashirikiana na wenzetu wa Kakonko kuona ni jinsi gani tufanye, lakini nikifahamu fika kwamba jana nilikuwa naongea na Wabunge wahusika wa maeneo haya na Mheshimiwa Mbunge pia na tuliona hata ikama ya Madaktari walioenda kule ni wachache na katika mchakato ule wa ajira zitakazokuja hapo baadaye tutaongeza idadi ya wataalam kwa sababu ukiachia miundombinu lakini suala la human resources ni jambo la msingi. Haya yote kwa Mkoa wa Kigoma tutayapa kipaumbele ili wananchi wa mkoa huu waweze kupata huduma za afya ya msingi.

Name

Freeman Aikaeli Mbowe

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Hospitali ya Vwawa Wilayani Mbozi inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitanda vya kulalia wajawazito pamoja na vile vya kujifungulia, pia wodi ya akinamama ni ndogo huku ukizingatia kuwa hospitali hiyo inahudumia Wilaya ya Mbozi na Momba:- Je, ni lini Serikali itajenga wodi ya akinamama kubwa yenye vifaa vya kutosha ili wanawake hawa waondokane na adha ya kulala wawili wawili?

Supplementary Question 3

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Tatizo linalowakabili wananchi wa Mbozi kwenye suala la Hospitali ya Wilaya kwa kiasi kikubwa linafanana na la Hospitali ya Wilaya ya Hai katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hospitali hii ya Wilaya ya Hai ilianza kujengwa zaidi ya miaka 10 iliyopita wakati huo Mji wa Hai ukiwa na wakazi wasiofika 10,000 na Mji wa Hai leo ni mji unaokua kwa kasi kuliko miji yote katika Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa katika kipindi cha miaka kumi, Mji wa Hai umefikisha zaidi ya wakazi 50,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali hii imekuwa inajengwa awamu kwa awamu lakini kuna tatizo moja kubwa la msingi ambako wanaume na wanawake wanalala katika wodi moja. Jambo hili nimeli-witness mwenyewe na nimetembelea hospitali hii wiki iliyopita kushuhudia hali hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachomwomba Naibu Waziri katika hatua ya sasa, kutokana na hali ya unyeti wa hospitali hii na ikiwa vilevile ni hospitali ambayo iko katika barabara kuu ya Arusha-Moshi ambayo inahudumia wagonjwa wote wanaopata ajali katika barabara ile, rai yangu kwa Mheshimiwa Waziri ni kutenga muda wake tuweze kutembelea pamoja hospitali hii kwa pamoja tuone uzito wa tatizo lililopo kisha Serikali itutafutie ufumbuzi wa kudumu kuhusu tatizo hili. (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba niseme takriban wiki tisa kama sio kumi zilizopita nilikuwa pale Hai. Nilienda kuitembelea hospitali ile na niliweza kubaini mchakato mkubwa unaofanywa na injinia wetu katika lile jengo la akinamama linalojengwa pale.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nimefarijika na nimefurahi sana kwa mkakati uliopangwa. Kwa kutumia hizi Force Account kazi kubwa inafanyika pale. Kwa hiyo, jambo la msingi ni kwamba kama Serikali pale kuna kazi kubwa tunaendelea kuifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme nimekubali wazo
hilo la kwenda pamoja lakini tayari nimeshakwenda na tumesha-identify na nimeshatoa maelekezo nini wanatakiwa wafanye. Namshukuru sana DMO wetu pale kwa kazi kubwa inayofanywa na menejimenti ya hospitali ile. Hata hivyo, nimetoa maagizo sasa waangalie rasilimali zilizokuwepo kama majengo yaliyokuwepo pale nini kifanyike, wapange mpango mzuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi kubwa tunayokwenda kufanya ni kukamilisha lile jengo kubwa linalojengwa ambalo ni la mfano na mimi nimetolea mfano hata nilivyokwenda Siha kule nikawaambia kwamba igeni kwa wenzenu wa Hai kwa kutumia Force Account, kutumia fedha ndogo na kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya afya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeweka nguvu kubwa pale. Hata hivyo, nina mpango wa kwenda Hai na Waziri wangu amepanga hilo kwa sababu Mheshimiwa Rais ameshaelekeza lazima tukahakiki suala zima la matumizi ya fedha na miundombinu ya barabara, kwa hiyo, tutakwenda tuone jinsi gani tutafanya ili hospitali ile iweze kuwahudumia vizuri wananchi wetu wa Hai.

Name

Richard Mganga Ndassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Hospitali ya Vwawa Wilayani Mbozi inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitanda vya kulalia wajawazito pamoja na vile vya kujifungulia, pia wodi ya akinamama ni ndogo huku ukizingatia kuwa hospitali hiyo inahudumia Wilaya ya Mbozi na Momba:- Je, ni lini Serikali itajenga wodi ya akinamama kubwa yenye vifaa vya kutosha ili wanawake hawa waondokane na adha ya kulala wawili wawili?

Supplementary Question 4

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Matatizo yaliyopo Mbozi Vwawa yanafanana sana na Kituo cha Afya cha Malya. Kituo cha Afya cha Malya kinahudumia Maswa, Malampaka na Kwimba. Kwa sababu Kituo cha Afya cha Malya kwa sasa kimezidiwa, miundombinu ya majengo na vyumba vya kusaidia wazazi havitoshi, Serikali ina mpango gani sasa wa kuwekeza angalau adha zilizopo pale ziweze kupungua?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, hii sehemu ya Kwimba ina Majimbo mawili, Jimbo la Mheshimiwa Ndassa na Mbunge mwingine lakini ukiangalia hospitali yetu ya wilaya na kule anakosema Malya ni kweli. Ndiyo maana naomba nimshukuru Mheshimiwa Mbunge, katika initiative zake za kutusumbua mimi na Waziri wa Afya alileta Kituo hiki cha Afya cha Malya kiweze kupewa kipaumbele.
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi TAMISEMI tumeshapitisha bajeti yetu na Wizara ya Afya imeshapitisha yao ni kwamba sasa hivi tunaenda kufanya uwekezaji mkubwa katika Kituo cha Afya cha Malya. Naomba nimhakikishie kwamba ombi lake kama Wizara ya Afya na Wizara ya TAMISEMI tumelichukua, tunaenda kufanya ukarabati mkubwa. Katika vile vituo 100 na Malya ni kimojawapo, tunaenda kuwasaidia wananchi wa jimbo lake.