Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Halima Ali Mohammed

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED aliuliza:- Kwa mujibu wa Ibara ya 19(1) ya Katiba ya nchi, kila mtu anayo haki na uhuru wa kuamini dini aitakayo, lakini pia chini ya Ibara ya 15(1) na (2) ya Katiba ni lazima sheria zifuatwe. Je, ni kwa nini wanawake wa kiislamu wanapovaa hijabu nikabu wanavuliwa na Maafisa Usalama wanaume?

Supplementary Question 1

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu ambayo hayaridhishi aliyotoa Mheshimiwa Naibu Waziri naomba sasa ni muulize maswali mawili ya nyongeza:
Kwa kuwa, wanawake wanaposafiri na kupitia bandarini kwenda Zanzibar au kutoka Zanzibar kuja Dar es Salaam wanavuliwa nikabu kuanzia katika geti la bandari, na kwa kuwa wanawake hawa wanapata manyanyaso na lugha za kejeli.
Je, ni muulize Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kupokea ushahidi?
Swali la pili, wapo wanaume wanaovaa mavazi na wakajipamba kujifananisha na wanawake, je, Serikali ina mpango gani wa kuwachukulia hatua wanaume hawa?(Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimezungumza katika jibu langu la msingi kwamba kama kuna matukio yoyote ambayo yameonekana kukiuka sheria za nchi ikiwemo hilo ambalo amelizungumza, kama ushahidi upo aulete tutaufanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa nikiri kwamba kuna baadhi ya maeneo kwa mfano, tulifanya ziara katika bandari ya Zanzibar tuliona utaratibu ambao unatumika katika kuwakagua abiria siyo mzuri na bahati nzuri tulikuwa na Naibu Waziri wa Miundombinu wa Zanzibar, hilo tumelizungumza na Serikali italifanyia kazi karibuni utaratibu ule utabadilika.Hata hivyo binafsi sikushuhudia wala kutokea malalamiko yoyote juu ya yale ambayo ameyazungumza Mheshimiwa Mbunge, lakini kama yapo na ushahidi upo basi tutafanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake la pili kwamba kuna wanaume wanavaa mavazi ya kike na wanawake wanavaa mavazi ya kiume. Tafsiri ya mavazi ya kiume na ya kike nayo ni tafsiri pana maana suruali ni vazi la kiume sijui tuliite la kike, mwanamke anavaa na mwanaume anavaa. Kwa hiyo, sidhani kama kuna tafsiri sahihi ya kusema hili ni vazi la kiume na ipi ni ya kike ili Serikali iingilie katika uhuru wa wananchi kuamua jinsi gani wanataka kuvaa ni uhuru wao Kikatiba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naona swali lake hili linahitaji kwenda ndani kidogo, limekosa ufafanuzi kwa hiyo linakosa majibu ya wazi ya moja kwa moja. (Kicheko)