Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU (K.n.y. MHE. HUSSEIN N. AMAR) aliuliza:- Ili viwanda viweze kufanya kazi kwa ufanisi vinahitaji malighafi ya kutosha. (a) Je, Serikali iko tayari kutoa bei ya pamba mapema kabla ya msimu wa kilimo kuanza ili wakulima wawe na uhakika wa bei elekezi? (b) Zao la pamba limekuwa na tatizo kubwa la mbegu zisizo bora na viuatilifu hafifu, je, Serikali imejipanga vipi kwa kuzingatia agizo la Mheshimiwa Rais la tarehe 31 Julai, 2016 alipokuwa akiongea na wananchi wa Geita kwamba hatavumilia kuona wananchi wakiletewa mbegu mbovu?

Supplementary Question 1

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Uhaba wa mbegu bora uliokuwepo mwaka 2015/2016 na kiwango kidogo cha ubora wa dawa ya pamba uliokuwepo mwaka 2015/2016 umeendelea kuwepo 2016/2017. Sasa swali langu la kwanza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri, ni kwa kiwango gani Wizara imejiandaa kumaliza tatizo hilo mwaka 2017/2018?
Swali langu la pili, wakati wa kampeni Mheshimiwa
Rais alipokuwa Kanda ya Ziwa aliagiza Bodi ya Pamba ihamie karibu na wazalishaji wa zao la Pamba. Sasa swali langu, ni kwa kiwango gani uwepo wa Bodi ya Pamba Kanda ya Ziwa umesaidia kuhakikisha kwamba zao hili la pamba linapata uzalishaji mkubwa? (Makofi)

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, kuhusu ni lini Serikali itaongeza kiasi au kiwango cha mbegu za pamba ili kukidhi mahitaji ya wakulima, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika msimu unaokuja wa kupanda pamba, tayari Bodi ya Pamba kwa kushirikiana na Mfuko wa Pamba wameweka mikakati kuhakikisha kwamba kutakuwa na mbegu za kutosha.
Mheshimiwa Spika, vilevile nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwamba siyo suala la kuongeza tu kiasi cha mbegu inayopatikana, lakini vile vile kuhusu ubora wake.
Mhshimiwa Spika, Bodi ya Pamba kwa kushirikiana
na Wizara na vituo vyetu vya utafiti, tayari kwa muda sasa tunafanyia utafiti mbegu aina ya UKM08 ambayo haina tatizo la ugonjwa wa unyaufu na hivyo tuko mbioni kuondokana kabisa na mbegu UK91 ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikileta usumbufu.
Mheshimiwa Spika, tunaamini kwamba tunapofikia mwaka 2018/2019 tayari mbegu hii mpya, yenye ubora ambayo haina magonjwa itakuwa imeingia sokoni na ifikapo mwaka 2020, mbegu aina ya UK91 itakuwa imeondoka sokoni moja kwa moja. Kwa hiyo, katika miaka hii michache inayokuja tutahakikisha kwamba tuneondokana kabisa na adha ya ugonjwa na ubora usio mzuri wa mbegu ya pamba.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu Bodi ya Pamba kuhamia katika maeneo ambayo yanazalishwa pamba, nimfahamishe tu kwamba agizo lile la Mheshimiwa Rais tayari limeshatekelezwa, Bodi ya Pamba wameshahamia Mwanza na kwa kiasi kikubwa tayari imesaidia sana kwa sababu watendaji wanaoshughulika na zao la pamba kila siku tayari wapo karibu nao. Kwa hiyo, inakuwa ni rahisi wao kuweza kufika katika Ofisi za Bodi za Pamba na kupata huduma, lakini vilevile watendaji wenyewe maana ni rahisi wao kufika katika maeneo ya wakulima na kutoa huduma zinazotakiwa.