Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Mohamed Keissy

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. ALLY K. MOHAMED (K.n.y. MHE. SILAFU J. MAUFI) Aliuliza:- Rukwa ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha mazao ya chakula hasa mahindi na mpunga kwa wingi na hivyo kusaidia upatikanaji wa chakula kwa Taifa. Maeneo mengi ya kilimo katika mkoa huo ikiwemo Bonde la Rukwa yanakabiliwa na changamoto ya barabara mbovu na hivyo wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao kwa wakati:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara za Kibaoni (Katavi) – Muze (Rukwa) – Kilyamatundu – Kamsamba (Songwe) hadi Mlowo, Sumbawanga – Muze, Kalambazite – Chambe (Ilemba) na Miangalua – Kilyamatundu (Kipeta) kwa kiwango cha lami ili wakulima wasafirishe mazao yao kwa urahisi?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, nakushuku sana. Kwanza naishukuru Serikali kusema kweli kutenga pesa za daraja kiungo muhimu sana kuhusu barabara. Hii barabara ni muhimu inaunganisha mikoa mitatu; Katavi, Rukwa na Songwe, ni muhimu kwa ajili ya wakulima wetu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka jibu sahihi, ni lini Serikali itakuwa tayari kujenga barabara ya lami katika mwambao wa Ziwa la Rukwa ili wananchi wafaidike? Atoe tarehe maalum, ni lini na mwaka gani? Maana hili daraja litajengwa, barabara inaweza ikaendelea hivyo hivyo kuwa tope wananchi wakateseka. Mwambao kule wanalima sana mazao muhimu sana. Kwa kuwa hii nchi ina njaa kila sehemu, tutakuwa tunakomboa sana wananchi wengine kutokana na mwambao wa Ziwa Rukwa kuwa na ardhi nzuri sana…
MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, hii
barabara inaanzia Mkoa wa Katavi, Kibaoni inakwenda mpaka Songwe kupitia Mwambao wa Ziwa Rukwa.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Ally Keissy ameuliza kwa sauti nzuri. Nikupongeze sana kwa hilo kwa sababu imenitia moyo.
Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Ally Keissy kwamba kama ambavyo nimejibu katika jibu la swali la msingi barabara hizi zote tunazitafutia fedha. Nimhakikishie kwamba procurement ya kupata mjenzi wa daraja la Kamsamba ambalo ndilo tunaanza nalo ni katika muda wa wiki mbili, tatu zijazo tutakuwa tumeshakamilisha. Ile hela ambayo ilitengwa mwaka huu itatumika na hatimaye mwaka unaofuata kwa hela hizi ambazo tumezitenga ambazo nilieleza toka mwanzo nazo tutakuwa tumekamilisha hii kazi itakuwa imekwisha.
Mheshimiwa Spika, baada ya hapo, sasa tunaenda kwenye barabara hizo.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. ALLY K. MOHAMED (K.n.y. MHE. SILAFU J. MAUFI) Aliuliza:- Rukwa ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha mazao ya chakula hasa mahindi na mpunga kwa wingi na hivyo kusaidia upatikanaji wa chakula kwa Taifa. Maeneo mengi ya kilimo katika mkoa huo ikiwemo Bonde la Rukwa yanakabiliwa na changamoto ya barabara mbovu na hivyo wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao kwa wakati:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara za Kibaoni (Katavi) – Muze (Rukwa) – Kilyamatundu – Kamsamba (Songwe) hadi Mlowo, Sumbawanga – Muze, Kalambazite – Chambe (Ilemba) na Miangalua – Kilyamatundu (Kipeta) kwa kiwango cha lami ili wakulima wasafirishe mazao yao kwa urahisi?

Supplementary Question 2

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, natambua jitihada ambazo zimefanyika kwenye hii barabara ikiwemo ujenzi wa daraja la Momba.
Mheshimiwa Spika, nataka tu niulize swali dogo, barabara hii imekuwa katika ahadi, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2009 alipokwenda kwenye Halmashauri ya Momba aliweka ahadi ya kujenga hii barabara. Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokwenda kule vilevile alitoa ahadi ya kuhakikisha hii barabara inakamilika kwa sababu hili bonde linaunganisha Mikoa mitatu na ni muhimu kwa mazao yetu.
Mheshimiwa Spika, Rais wa Awamu ya Tano Mheshimiwa John Pombe Magufuli alisema katika Serikali yake hataki kusikia mambo ya michakato, ahadi, tunatafuta fedha, alisema mwenyewe. Watu wa Mikoa wa Songwe, Rukwa pamoja na Katavi tumekuwa tukilia kila mwaka ni kwa nini sasa mwaka huu msiweke commitment katika barabara zote mkatenga tu fedha kuelekeza katika Mkoa huu wa Rukwa, hususan hii barabara kutoka Mlowo mpaka Kamsamba na Kilyamatundu kwa kiwango cha lami ili tuache
kuwasumbua tena katika kipindi cha miaka mitano. Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, nikuhakikishie barabara ya Mbande – Kongwa tunaijenga. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba kumhakikishia
Mheshimiwa Silinde kwamba daraja la Kamsamba nadhani maswali yake yote ya nyuma yalikuwa yanaelekea hapo. Umeona kwamba sasa hii siyo ahadi tena tunatekeleza, siyo michakato, tunatekeleza. Kabla hujatekeleza taratibu za usanifu, upembuzi lazima zifanyike vinginevyo huwezi ukatekeleza. Kwa hiyo, hatua ya kwanza ya kufanya usanifu wa kina na upembuzi yakinifu tunaianza kwa kutafuta fedha na mara tutakapopata fedha, kazi hii tutaanza. Suala siyo
michakato hapa tutatekeleza kama tulivyoahidi.