Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joram Ismael Hongoli

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupembe

Primary Question

MHE. JORAM I. HONGOLI (K.n.y. MHE. EDWARD F. MWALONGO) aliuliza:- Uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na mifuko ya plastiki ni mkubwa mno nchini:- (a) Je, Serikali haioni sasa umefikia wakati wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo? (b) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwawezesha wadau wa mazingira kwa kuwanunulia mashine kwa mkopo ili waweze kuchakata plastiki hizo kuzifanya kuwa ngumu na bora zaidi?

Supplementary Question 1

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza swali moja tu la nyongeza.
Je ni lini sasa Serikali itaanza kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara yanayotokana na hii mifuko ya plastiki?

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, tunaanza leo kutoa elimu ya uzingatiaji wa matumizi ya mifuko ya plastiki, wananchi waweze kuzingatia hilo, Sheria na kanuni hii yetu ya 2015 kwamba matumizi ya plastiki ambayo yanayoruhusiwa ni yale tu yenye makroni 50. Kwa hiyo, ni jukumu la Bunge hili na Wabunge wote, wadau wote na wazalishaji na wenye viwanda kuchukua jukumu na kuhakikisha kwamba plastiki zinazozalishwa ni zile tu zenye makroni 50 ambazo ndizo zimeruhusiwa na Kanuni, zaidi ya hapo hairusiwi na haikubaliki na watu watakaoenda kinyume watachukuliwa hatua kali za kisheria, tutachukua hatua kali kwenye viwanda ambavyo vitazalisha zaidi ya kiwango hiki kilichoruhusiwa ikiwa ni pamoja na kufunga kabisa viwanda hivyo. Hatutaruhusu matumizi hayo kwa namna yoyote yatumike nchini. Kwa hiyo, ni jukumu la Bunge hili, ni jukumu la wananchi wote, kuelewa kwamba plastiki iliyoruhusiwa ni ile yenye makroni 50 peke yake.