Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mattar Ali Salum

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shaurimoyo

Primary Question

MHE. MATTAR ALI SALUM Aliuliza:- Kuna malalamiko makubwa kwa upande wa Zanzibar kuhusu idadi ndogo ya wanafunzi wanaopata Mkopo wa Elimu ya Juu jambo ambalo linapunguza idadi ya wataalamu kwa upande wa Zanzibar, hivyo kuingia katika soko la ajira katika Afrika ya Mashariki na Kati na kuijenga nchi yetu kwa ujumla. (a) Je, Serikali haioni kuwa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Juu inatakiwa kutenga asilimia maalum kwa wanafunzi kutoka Tanzania Zanzibar? (b) Je, bajeti iliyotengwa kwa mwaka huo wa 2015/2016 ni kiasi gani?

Supplementary Question 1

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mweyekiti, ahsante sana kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nisawazishe jina langu, mimi naitwa Mattar Ali Salum, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri akilijibu alijibu vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake ambayo ameyatoa.
Mheshimiwa Waziri, wapo wanafunzi wanaendelea kupata mikopo ya Serikali kwa kima kidogo hadi sasa, husababisha kukosa kukidhi mahitaji ya vyuo husika ambavyo wamepangiwa. Je, Serikali ni kwa nini isiwaongezee fedha wanafunzi hawa ili waweze kukidhi mahitaji ya vyuo husika?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wako wanafunzi walikuwa wakipata mikopo kwa kipindi kirefu, ghafla Serikali imewafutia mikopo yao, sijui ni kwa nini. Je, Mheshimiwa Waziri, Serikali ina mpango gani wa kuwarejeshea mikopo hawa wanafunzi ili waweze kukidhi na kuendelea na masomo yao vizuri? Ahsante sana.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama alivyorekebisha jina lake, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba kiuhalisiatulingependa kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi, lakini vilevile ingewezekana hata kila mwanafunzi akapata mkopo kwa kadiri ya mahitaji ya chuo anachosoma; lakini kwa sababu fedha hazitoshi inakuwa ni vigumu kufanya hivyo na tunaangalia zaidi ni uhitaji wa kiasi gani upo.
Kwa hiyo, kwa misingi hiyo niseme tu kwamba, Serikali itaendelea kutenga fedha ya kuona kwamba, inawasaidia wanafunzi wengi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusu kufuta mikopo. Ni kweli kuna baadhi ya wanafunzi walifutiwa mikopo kutokana na kutokuwa na vigezo vinavyostahili. Hata hivyo Serikali imeendelea kulifanyia kazi suala hilo ili kuona kwamba, anayefutiwa mkopo iwe kweli ni mtu ambaye hana uhitaji. Kwa yule mwenye uhitaji na kwamba vigezo vyote vimetimia basi, baadhi yao tumeweza pia kuwarejeshea.