Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Machano Othman Said

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko ya wananchi, watumishi wa umma na wafanyabiashara juu ya riba kubwa inayotozwa na benki zetu kwa wale wanaochukua mikopo hali ambayo inarudisha nyuma juhudi zao za kupunguza umaskini na kwa kuwa Benki Kuu ndiyo inayosimamia mabenki yote nchini. (a) Je, ni lini Serikali kwa kupitia benki zetu nchini itaweka utaratibu wa kupunguza riba ya mikopo walau kufikia 10% -12% badala ya riba ya sasa ambayo ni 17% - 20%? (b) Kwa kuwa mikopo inayotolewa kwa watumishi wa umma ni salama zaidi kwa mabenki, je, benki hizo haziwezi kuweka riba maalum?

Supplementary Question 1

MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha, naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza ni kwamba kutokana na kwamba hii Sheria ya Fedha ipo kwa muda mrefu tangu mwaka 1991, na kutokana na mabadiliko ya kidunia ya uchumi na baadhi ya nchi jirani kubadilisha sheria hizi katika nchi zao; je, haaoni kwamba umefika wakati kwa Serikali kubadilisha sheria hii?
Na la pili, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba riba katika mwezi wa Juni, 2016 ilikua kwa kiwango cha 13.46 lakini ukweli halisi ilikuwa ni kati ya 16 mpaka 18. Katika swali langu niliuliza je, haoni kwamba Serikali inahitaji ichukue juhudi maalum kwa wafanyakazi wa Serikali kwa sababu fedha zao kulipwa ni rahisi na zina dhamana zaidi, anaonaje Mheshimiwa Waziri?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza anauliza utayari wa Serikali kubadilisha sheria, naomba nilikumbushe Bunge lako Tukufu, tuko katika soko huria na tunafuata soko huria hivyo haiwezekani kurudi katika kuelekeza mabenki yetu. Kama nilivyosema katika jibu langu la msingi, Benki Kuu ikifanya hivyo itakosa mamlaka sasa ya kuyasimamia mabenki hayo pindi yatakapopata hasara kutokana na riba elekezi iliyoyatoa. Hivyo nashauri tu tuendelee na mfumo uliopo kwa sababu tupo katika mfumo wa soko huria na hii pia ni global practice hivyo siamini kwamba ni njia njema kwa nchi yetu kuweza kurejea katika maelekezo kwa ajili ya riba zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, naomba niseme kwamba kuhusu kutoa riba elekezi kwa wafanyakazi pia haiwezekani kwa sababu riba tunazoziona zinakuwa ni wastani wa riba ambazo zimetolewa kutoka katika sekta na makundi mbalimbali, hivyo tukisema wafanyakazi tuwape riba nafuu itapelekea makundi mengine ambayo hasara yake au vihatarishi ni vya juu kupata riba kubwa sana na hivyo tutakuwa tumewaumiza.
Kwa hiyo, niliombe Bunge lako Tukufu na Wabunge kwamba tukubaliane na wastani huo ambao hutolewa na Benki Kuu baada ya kupata sasa riba zote kutoka katika mabenki yetu yote.

Name

Maryam Salum Msabaha

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko ya wananchi, watumishi wa umma na wafanyabiashara juu ya riba kubwa inayotozwa na benki zetu kwa wale wanaochukua mikopo hali ambayo inarudisha nyuma juhudi zao za kupunguza umaskini na kwa kuwa Benki Kuu ndiyo inayosimamia mabenki yote nchini. (a) Je, ni lini Serikali kwa kupitia benki zetu nchini itaweka utaratibu wa kupunguza riba ya mikopo walau kufikia 10% -12% badala ya riba ya sasa ambayo ni 17% - 20%? (b) Kwa kuwa mikopo inayotolewa kwa watumishi wa umma ni salama zaidi kwa mabenki, je, benki hizo haziwezi kuweka riba maalum?

Supplementary Question 2

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, na mimi naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri swali dogo la nyongeza.
Kwa kuwa wajasirimali wadogo wadogo hasa mama lishe na wamachinga na ambao wengine wana vipato vya chini wamekuwa wakikopa mikopo kwa ajili ya biashara zao na kutozwa riba kubwa na kushindwa kurejesha mikopo ile na kufilisiwa.
Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha inatafuta fedha kwa ajili ya Wajasiriamal wadogo wadogo na kuwatoza riba ambayo inaendana na biashara zao?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nilikumbushe Bunge lako tukufu kwamba tayari Serikali imeshatunga sera ya huduma ndogo za fedha za mwaka 2016 na sasa tupo katika hatua nzuri kuja na sheria katika Bunge lako tukufu ili kuwalinda wajasiriamali wadogo wanaokopeshwa kwa riba kubwa. Ni imani yangu sheria hii itakapokuwa imepitishwa watakopa katika viwango halisi ambavyo viko sokoni na sivyo ambavyo wanaonewa kwa sasa.