Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mgeni Jadi Kadika

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MGENI JADI KADIKA aliuliza:- Serikali inajitahidi kujenga na kuimarisha madaraja ili kuondoa kero na kupunguza maafa; Daraja la Mto Wami lililopo barabara ya Tanga ni jembamba sana kiasi kwamba magari mawili hayawezi kupishana kwa wakati mmoja:- Je, Serikali ina mpango gani wa kulipanua daraja hilo la Mto Wami?

Supplementary Question 1

MHE. MGENI J. KADIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya nyongeza, ninayo maswali mawili. Kwa kuwa Serikali inaitisha zabuni mwezi wa Februari kama ilivyosema na imetenga shilingi bilioni tatu kwa mwaka wa fedha 2016/2017: Je, Serikali haioni kuwa ni muda mfupi unaobakia mpaka kumalizika bajeti? Je, daraja hilo kweli litajengwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili: Je, Serikali haioni kuchelewesha kujenga daraja hilo ni kuzorotesha maendeleo na kuongezeka kwa ajali na hicho ndiyo kilio cha watu wa Tanga?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba kumhakikishia Mheshimiwa Jadi Kadika kwamba huo muda unatosha sana. Taratibu ni lazima zifuatwe kabla ujenzi haujaanza. Kwa hiyo, hatua za kwanza zilikuwa ni kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na hatimaye kuandaa nyaraka za zabuni, kazi hiyo tumeikamilisha. Sasa mwezi wa Pili, tunaitisha tenda na mambo yakikamilika tukampata mkandarasi, hiyo shilingi bilioni tatu itatoka na kazi ya ujenzi itaanza.