Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yussuf Salim Hussein

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chambani

Primary Question

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN aliuliza:- Karibu theluthi moja ya ardhi ya Tanzania ni misitu na kuna uhaba mkubwa wa watalaam wa misitu nchini. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha Chuo cha Misitu cha Olmotonyi? (b)Je, kila mtalaam wa misitu aliyepo leo anasimamia hekta ngapi za eneo?

Supplementary Question 1

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri ambayo anajitetea na kijificha katika msitu wa njugu. Ni-declare interest mimi ni mtaalam wa misitu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilichouliza ninataka kujua Serikali ina mkakati gani mahsusi wa kuongeza idadi ya wanafunzi katika chuo kile ili kukabiliana na paragraph ya mwanzo ya majibu yako. Ieleweke kwamba tunaposema wataalam wa misitu (foresters) hasa ni wale certificate na diploma kwa sababu wale ndiyo field officers na kukosekana kwa wale ndiyo sasa hivi deforestation imeongezeka na afforestation imepungua.
Mheshimiwa Spika, nataka kujua mkakati upi wa Serikali wa kuongeza idadi ya wanafunzi wa certificate na diploma katika chuo kile ili kukabiliana na hali hii tuliyonayo katika nchi yetu ya uharibifu wa misitu na mazingira? (Makofi)
Swali la pili, mheshimiwa Waziri, Chuo cha Misitu cha Olmotonyi katika miaka ya 1980 kilikuwa na hadhi ya Kimataifa, sijui leo; na kilikuwa kinapokea wanafunzi kutoka nje ya nchi. Je, Serikali inasema nini katika kukiboresha chuo hiki kikaendelea kupokea wanafunzi kutoka nje ikawa ni moja kati ya source of income za Serikali hii, kuipatia fedha za kigeni? Nashukuru!

Name

Prof. Jumanne Abdallah Maghembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Answer

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Yussuf kwa maswali yake mazuri.
Mheshimiwa Spika, kwanza ni uwezo wa chuo kuongeza wanafunzi na katika jibu la msingi hapa, tumepanua chuo ili kiweze kuwa na hall ya mhadhara mmoja ambao unaweza sasa kubeba wanafunzi 200 kwa wakati mmoja. Tumepanua na nafasi nyingine na hasa kuboresha maktaba ili iwe bora zaidi na iweze kuwa na rasilimali za vifaa vya kujifunzia bora zaidi. Kwa kufanya hivyo tunaweza kuongeza wanafunzi wengi zaidi na kufanya chuo kitoe mafunzo mazuri zaidi.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba huko nyuma, Chuo cha Olmotonyi kilikuwa kinachukua wanafunzi kutoka nje ya nchi, lakini katika ngazi hii ya cheti na ngazi ya diploma, hii ni ngazi ya msingi sana kama elimu ya msingi kwenye mafunzo haya ya misitu.
Mheshimiwa Spika, katika mafunzo haya ya misitu nchi nyingi ambazo zilikuwa zinaleta wanafunzi kwetu zimejijengea uwezo wake wa kutoa mafunzo ya msingi. Siku hizi wanafunzi wa Kimataifa wanakuja kusoma kwenye chuo chetu cha misitu kilichopo kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ambacho ndicho chuo bora zaidi kwenye fani ya misitu kuliko vyuo vyote Barani Afrika.