Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Primary Question

MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:- Kutokana na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea hivi sasa duniani pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira Mkoa wa Simiyu ni moja kati ya maeneo yaliyoathirika kwa kiwango kikubwa na kuna uwezekano mkubwa wa Mkoa huo kugeuka kuwa jangwa:- (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa makusudi wa kuunusuru Mkoa huo na hali hiyo; (b) Kwa kuwa, hali hiyo inaathiri shughuli za kilimo hasa cha umwagiliaji; je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha mazingira ya mito na mabwawa yanatunzwa?

Supplementary Question 1

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Pamoja na mikakati na Sheria na Sera za Kitaifa za Mazingira ya Mwaka 1997, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, Mkakati wa Hatua za Kuhifadhi Mazingira 2008, pamoja na Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2012. Swali langu la nyongeza dogo, Serikali ina mpango gani maalum kwa Mkoa huu wa Simiyu kwa sababu hizi sheria na mikakati yote inaonekana ni ya Kitaifa zaidi? Ninachotaka ni kupata commitment ya Serikali maalum kwa Mkoa huu wa Simiyu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mkoa wa Simiyu kweli unategemea kupata maji kutokana na huu mradi wa Simiyu Resilient Development Programme wa kutoka Ziwa Victoria, lakini katika Mkoa huu Maswa itapata maji katika mradi huu katika phase ya pili. Vilevile jibu la Mheshimiwa Naibu Waziri linasema kwamba utekelezaji wa kupata maji maeneo haya kutoka Ziwa Victoria unatekelezwa na Wizara ya Maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba commitment ya Wizara ya Maji, ni lini itafufua mabwawa ya Wilaya ya Maswa kwa sababu itachelewa kupata maji. Kuna mabwawa mengi zaidi ya mabwawa 35 na yamefanyiwa upembuzi yakinifu yanahitaji shilingi bilioni 1.2 tu kufufuliwa ili watu waweze kupata maji na waweze kuotesha na kumwagilia miti yao. Nashukuru.

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mazuri. Mradi huu pia unapita kwenye jimbo lake la uchaguzi na vilevile unapita kwenye jimbo langu la uchaguzi. Napenda kuwahakikishia wananchi kwamba, mpango maalum ambao Mheshimiwa ameuzungumza hapa, ambao nataka kumwambia mpango maalum wa kunusuru Mkoa wa Simiyu ndiyo huu sasa wa mradi mkubwa kabisa wa Kitaifa ambao utagharimu Euro milioni 313. Serikali tunatarajia kuanza ujenzi huu ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017, tunatarajia tuwe tumeanza ujenzi wa mradi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia kwamba mradi huu umo ndani ya Ilani ya uchaguzi, lakini commitment ya Serikali na Mheshimiwa Rais aliahidi kwamba lazima utekelezwe katika kipindi hicho. Mipango mingine ya Serikali inaenda yote kwa pamoja, tulizungumza hapa katika mpango wetu kwamba tumeanzisha Mfuko wa Mazingira sasa ambao tuna uhakika kwamba tutapata fursa nzuri ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi lakini tutapata fursa tena nyingine nzuri sana ya kuhakikisha kwamba tunapambana na uharibifu wa mazingira na kwamba tutaziimarisha taasisi zinazohusika katika usimamizi wa mazingira ili ziweze kusimamia mazingira vizuri zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo Mheshimiwa ameuliza hapa, ni kwamba, kuna mabwawa ya maji katika Wilaya ya Maswa ambayo kwamba hayako kwenye hali nzuri na kwa kweli yanahitaji kufufuliwa. Katika hatua hii ninachoweza kusema kwamba wataalam wa ofisi yangu ya mazingira pamoja na wa Wizara ya Maji watakwenda kufanya tathmini na kuona namna bora ya kufufua mabwawa haya ili kuhakikisha kwamba wananchi wa Wilaya ya Maswa Mashariki la Mheshimiwa Nyongo wanapata maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ya uchumi.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongeze majibu ya nyongeza, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri kuhusu commitment ya Serikali kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuendeleza yale mabwawa ambayo tumeainisha mabwawa 35.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukirejea bajeti yetu tumeweka bilioni sita, fedha za ndani kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji. Kwa hiyo, yapo mabwawa ambayo tumeyaainisha katika Mkoa wa Simiyu ambayo yatashughulikiwa na bajeti hii katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.