Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca David Kishoa

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwa na habari za uamuzi wa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa upepo Mkoa wa Singida:- Je, ni lini mradi huo utatekelezwa?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa mujibu wa jarida la The Citizen la tarehe 23, Oktoba mwaka huu, 2016, imeonyesha kwamba miongoni mwa mikopo iliyokopwa kutoka China mwaka 2015 ni pamoja na Dola za Kimarekani milioni 132 ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 300 za Kitanzania kwa ajili ya mradi wa umeme wa upepo Singida.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali iwaeleze wananchi wa Singida fedha hizi zimekwenda wapi? Kwa sababu mpaka hivi sasa hakuna kinachoendelea, hakuna hata nguzo moja halafu tunaambiwa bado majadiliano yanaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa sababu mazingira kama haya ambapo mikopo inaombwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini fedha zinaelekezwa maeneo yasiyohusika. Ni lini Serikali itaona kuna umuhimu wa kumwagiza CAG akague mikopo inayoagizwa katika nchi hii? Kwa sababu katika deni la Taifa, inawezekana kuna ujanja ujanja unafanyika kwenye suala zima la mikopo. Ahsante.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa mradi wa upepo wa Singida ambao unazalisha Megawatt 100 hautokani na fedha za mkopo, ni wawekezaji binafsi, niweke wazi. Kadhalika, kuhusiana na masharti ya mikopo, ni Makampuni yenyewe yanakopa na kuja kuwekeza kwa ajili ya kufanya biashara na TANESCO inanunua umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la CAG, ni taratibu za Kiserikali. CAG ana utaratibu wa kukagua na Mashirika na ofisi za Serikali zina utaratibu wa kuwasilisha taarifa za kukaguliwa. Tutaendelea kupeleka taarifa kwa mujibu wa CAG ili hesabu zote zikaguliwe. Kwa hiyo, hakuna suala la kuficha kwenye ukaguzi; CAG ana ratiba ya kukagua na Serikali tuna wajibu wa kupeleka takwimu ili zikaguliwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea kupeleka takwimu zikaguliwe.