Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Khadija Nassir Ali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KHADIJA NASSIR ALI aliuliza:- Tanzania tunalima pamba kwa wingi lakini bado tunaagiza Gauze toka Uganda ambao hawana zao la pamba, lakini pia tunaagiza Drip toka nje ya nchi wakati tuna maji ya kutosha ya kuweza kutengeneza Drip hizo:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutumia malighafi hizo ili kuzalisha Gauze na Drip hapa nchini na kuacha kuagiza bidhaa hizo toka nje?

Supplementary Question 1

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Ikizingatiwa azma ya kujenga Tanzania ya viwanda, ni lini Serikali itajenga viwanda hivi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa nini Serikali isiwekeze kwenye kujenga viwanda vidogo vya drip kwenye hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili ku-supply drip kwenye hospitali husika kama ilivyokuwa zamani badala ya kuagiza drip hizo nje ya nchi jambo ambalo ni aibu kwa Taifa letu? Ahsante.

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunajenga viwanda na niwatoe wasiwasi Wabunge wenzangu kuna kampuni mbili za media zimekubali kunisaidia kujibu maswali ya Wabunge kuanzia kesho. Wataonesha vipindi vyote, kiwanda hiki Mwijage naonyesha, hiki kinajengwa hiki kinajengwa. Hata hivyo, kwenye swali langu la msingi nimeorodhesha makampuni ambayo nimehamasisha, nimepiga sound, wakaja kuomba kuwekeza. Kwa hiyo kazi yangu ndiyo hiyo, nimeeleza viwanda vyote hivi wamekuja kuwekeza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa nini hospitali ndogo zisitengeneze drip. Nimshukuru Mheshimiwa Khadija, hospitali za kwetu nchini ukienda Tabora, Kagondo, Bugando wanatengeneza drip. Nitumie fursa hii kama kuna hospitali yoyote ambayo inataka kwenda kupata ile mitambo ya kutengeneza drip iwasiliane na Wizara ya Afya tuna utaratibu maalum. Viwanda vya kutengeneza drip siyo pesa za ajabu, ndiyo vile viwanda wanavyosema Mwijage anatembea navyo mfukoni, kweli ninavyo.