Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Desderius John Mipata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuza:- Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Rukwa ilishaomba juu ya barabara za Kitosi – Wampembe na Nkana – Kala kuchukuliwa na Mkoa na Serikali imeendelea kuzifanyia matengenezo ya dharura ili zipitike na kilio cha barabara hizo kilifikishwa kwa Rais pamoja na Makamu wa Rais wa Awamu ya Tano na wote walitoa ahadi ya kuboresha barabara hizo:- (i) Je, Serikali ina mpango wowote wa kuzipandisha hadhi barabara hizo? (ii) Je, ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi wanaopata shida kwa barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka?

Supplementary Question 1

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nina maswali mawili ya nyongeza. Barabara ya Nkana – Kala mwishoni mwa mwaka jana ilijifunga na ikalazimika kutafuta fedha za dharura zaidi ya milioni 400 ambazo Serikali iliipatia na tukapeleka ndiyo ikafunguka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi imefanyika vizuri, naishukuru sana Serikali. Hata hivyo, lipo tatizo kwamba tusipopeleka pesa kwa sasa hivi kwa jiografia ya barabara zile ambazo zinaenda mwambao mwa Ziwa Tanganyika kwenye miporomoko, juhudi kubwa iliyofanyika na Serikali mwaka huu, haiwezi kulindwa na fedha kidogo iliyotengwa na Halmashauri ndiyo maana tuliomba fedha pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiuliza Serikali, je, inakubaliana na ushauri wangu kwamba ili kulinda fedha zilizotumika mwaka jana inatakiwa ipeleke pesa nyingine zaidi kwa barabara hii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, iko barabara ya Kasu – Katani – Chonga – Chalatila – Myula na ile ya Kisula - Milundikwa na Malongwe. Barabara hizi ni za Halmshauri, zimekuwa zikijifunga kila wakati na sababu kubwa ni hiyo hiyo ya Halmashauri kuwa na pesa kidogo. Ni lini Serikali itaongeza pesa kwa Halmashauri ili ziweze kumudu kutengeneza barabara katika viwango vinavyohitajika?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika swali langu la msingi, hizi barabara na mazingira ya mvua tunayokuwa nayo katika misimu ya mvua siyo rahisi kuahidi kwamba, barabara hii pekee tupeleke fedha kiasi hiki. Tatizo linapotokea Serikali inashughulikia chini ya Mfuko wa Dharura ambao upo katika kila TANROAD Mkoa. Naomba tuvumiliane kwa mazingira tuliyonayo, Serikali itaendelea kuongeza juhudi, kuhakikisha inatekeleza wajibu wake wa kuhakikisha mawasiliano sehemu zote za nchi yanapatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili, naomba hizi barabara tukaziangalie upya na ziletewe maombi kama ambavyo hizi zingine zililetewa ili Wizara yetu iweze kuzitathmini na kuangalia vigezo vile kama vinakidhi kupandisha hadhi au kuviongezea fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnafahamu kwamba fedha zilizoko ni zile ambazo zinapangwa hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge uwezo tunaopewa ni ule ambao Bunge linaidhinisha na kiwango kile tunachopata kupitia Road Board ndicho kinachogawiwa kwa nchi nzima.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuza:- Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Rukwa ilishaomba juu ya barabara za Kitosi – Wampembe na Nkana – Kala kuchukuliwa na Mkoa na Serikali imeendelea kuzifanyia matengenezo ya dharura ili zipitike na kilio cha barabara hizo kilifikishwa kwa Rais pamoja na Makamu wa Rais wa Awamu ya Tano na wote walitoa ahadi ya kuboresha barabara hizo:- (i) Je, Serikali ina mpango wowote wa kuzipandisha hadhi barabara hizo? (ii) Je, ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi wanaopata shida kwa barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka?

Supplementary Question 2

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Ukarabati wa barabara pia unaendana na utanuzi wa barabara. Serikali ilikuwa inatanua barabara kuu ya kutoka Mwanza kwenda Musoma na ilifuata nyumba za wananchi na wakawafanyia tathmini, lakini kwa bahati mbaya mpaka leo hawajalipwa na kuna wazee wangu kule wanapata taabu sana, nyumba zao hazijalipwa na wanaishi kwa taabu. Miongoni mwa wazee wangu ni pamoja na baba yangu Mzee Wasira, naye nyumba yake imefanyiwa tathmini katika kijiji chetu cha Manyamanyama.
Je, ni lini mtawalipa wananchi wa Bunda kwa sababu mmeshawafanyia tathmini miaka mitatu iliyopita?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
MWENYEKITI: Lini mtawalipa.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Fedha zitakapopatikana tutawalipa.