Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Othman Omar Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. OTHMAN OMAR HAJI aliuliza:- Kwa kuzingatia usalama na utulivu wa nchi yetu, viongozi wa Serikali wamekuwa wakitoa kauli zenye msisitizo kwa wananchi kuepuka kuhubiri siasa katika nyumba za ibada na kuchanganya dini na siasa katika mikutano. Je, ni kifungu gani cha Katiba au Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambacho kinafafanua juu ya kauli hizo?

Supplementary Question 1

MHE. OTHMAN OMAR HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, iwapo itatokea kiongozi wa Umma atazungumzia masuala ya kisiasa ndani ya nyumba ya ibada; je, ni kifungu gani cha katiba au sheria kinachoweza kumtia hatiani kiongozi huyu? (Makofi)
Swali la pili, iwapo katika matamshi yake aliyoyazungumza katika nyumba hiyo inakwaza jamii moja katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania.
Je, ni adhabu gani amestahiki Kiongozi kama huyu? (Makofi/Kicheko)

Name

Dr. Harrison George Mwakyembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nilishaeleza katika jibu langu la swali la msingi kwamba mtu yeyote ambaye atafanya kinyume na ambacho Katiba inaelekeza na vilevile sheria, atakuwa amefanya makosa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nisisitize tu hapa kwamba, Katiba ya nchi ndiyo inayozaa sheria. Kwa hiyo, siyo siyo tu mtu, hata chama cha siasa ambacho kinaendekeza masuala ya kidini nacho kinakuwa kimekosea, lakini siyo suala la mtu mmoja kuamua kuwa umekosea, kuna utaratibu wa kuweza kulifikisha hilo suala mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hatua za kisheria kuweza kuchukuliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo hivyo kwa viongozi wa Kiserikali, anaingia kwenye Kanisa au Msikitini, siyo Serikali iweze yenyewe kuwa kila sehemu, lakini ijengwe hoja na wananchi ambao wamefika pale na huko ndiko kulinda utawala wa sheria katika nchi yetu. (Makofi)