Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA (K.n.y. MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA) aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Muleba in shule 39 za sekondari za kata na kati ya hizo, shule 31 hazina walimu wa vipindi muhimu na nyingine zina walimu wa ziada wasio na kazi; mfano shule 12 hazina walimu wa hesabu kabisa, shule tisa baiolojia, shule nane kemia, shule 18 walimu wa fizikia na shule 10 hazina kabisa walimu wa uraia. (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kukabiliana na tatizo hilo na kuliondoa ili kuokoa kizazi cha vijana watakaoishi katika karne ya 21 bila kusoma masomo ya sayansi? (b) Je, kuhusu walimu wa ziada takribani 213 wasiohitajika kwenye sekondari kwa sasa hivi, Serikali itaruhusu Halmashauri iwapange kufundisha kwenye shule za msingi ambapo kuna upungufu mkubwa kuliko kuingia gharama kuwahamisha na kuwarejesha tena wakihitajika kwa sababu shule za sekondari zinaendelea kupanuka? (c) Je, Serikali itasaidiaje Halmashauri ya Muleba kutengeneza programu maalum ya mafunzo kwa walimu wa ziada kujifunza kufundisha masomo mengine ambayo walimu wake hawatoshi?

Supplementary Question 1

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kujibu maswali vizuri, lakini tunajua kabisa kwamba kuna tatizo kubwa sana la walimu wa sayansi katika Wilaya zote. Sasa je, Serikali ina mkakati gani wa kuchagua chuo kimoja kuweza kusomesha walimu wa sayansi tu? Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Mkwawa pale, tungeamua kitoe masomo ya sayansi ili tuweze kupata walimu wengi?
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kwa nini Serikali sasa isitoe mkopo kwa asilimia mia moja kwa wale wanafunzi ambao wanasomea masomo ya sayansi ili kuwavutia wanafunzi waweze kujiunga na ualimu wa sayansi? (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la mkakati wa kuwapata walimu wa sayansi, kama unavyofahamu kwamba tayari Serikali ilishachukua hatua na kama mnavyokumbuka kwamba tulikuwa na wanafunzi zaidi ya 7,800 ambao walikuwa katika Chuo cha UDOM ambao kwa sasa tumewatawanya katika vyuo mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wale ambao wana vigezo sasa hivi kwa kufundisha shule za sekondari ni zaidi ya walimu 6,305 wakishamaliza masomo yao wataweza kwenda kwenye hizo shule. Kwa hiyo, Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kufundisha walimu wa sayansi na wakati huo huo kuhakikisha kwamba maabara kwa ajili ya shule za sekondari ili kupata wanafunzi wengi zaidi katika maeneo ya sayansi yaweze pia kukamilika na kupewa vifaa vinavyostahili.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA (K.n.y. MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA) aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Muleba in shule 39 za sekondari za kata na kati ya hizo, shule 31 hazina walimu wa vipindi muhimu na nyingine zina walimu wa ziada wasio na kazi; mfano shule 12 hazina walimu wa hesabu kabisa, shule tisa baiolojia, shule nane kemia, shule 18 walimu wa fizikia na shule 10 hazina kabisa walimu wa uraia. (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kukabiliana na tatizo hilo na kuliondoa ili kuokoa kizazi cha vijana watakaoishi katika karne ya 21 bila kusoma masomo ya sayansi? (b) Je, kuhusu walimu wa ziada takribani 213 wasiohitajika kwenye sekondari kwa sasa hivi, Serikali itaruhusu Halmashauri iwapange kufundisha kwenye shule za msingi ambapo kuna upungufu mkubwa kuliko kuingia gharama kuwahamisha na kuwarejesha tena wakihitajika kwa sababu shule za sekondari zinaendelea kupanuka? (c) Je, Serikali itasaidiaje Halmashauri ya Muleba kutengeneza programu maalum ya mafunzo kwa walimu wa ziada kujifunza kufundisha masomo mengine ambayo walimu wake hawatoshi?

Supplementary Question 2

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.
Kwa kuwa Serikali imetangaza kwamba nchi yetu sasa masomo ya sayansi ni lazima kwa wanafunzi wetu; lakini hakuna maandalizi ambayo yamefanyika mpaka sasa, hatuna walimu hao kabisa. Nitolee mfano katika Jimbo langu la Babati Mjini, walimu wa mathematics katika shule kumi za sekondari, ni shule moja tu ndiyo ina mwalimu wa hesabu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nifahamu, Serikali haioni kwamba inawachanganya wananchi wa Tanzania katika kutoa kauli zao wakati hawajajiandaa kukabiliana na tatizo hilo? Ni lini wanaajiri walimu hao wa sayansi? (Makofi)

Name

Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme kwamba wanafunzi kusoma sayansi kama somo la lazima halijaanza, lakini Serikali iko katika maandalizi. Hatua muhimu ambayo imefanyika ni kuhakikisha kwamba kila shule inakuwa na maabara ambapo hizi maabara tunashukuru kwamba zimejengwa kwa ushirikiano na wananchi hatua inayofuata, sasa hivi Serikali ipo katika utaratibu wa kuhakikisha kwamba maabara zote za sayansi zilizojengwa kwenye shule za sekondari zinakamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali wa kwamba masomo ya sayansi yatakuwa ni ya lazima, unaendana sambamba na Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ambapo elimu inakuwa ya msingi kwamba wanafunzi wanasoma kuanzia msingi mpaka sekondari. Kwa hiyo, Serikali bado ipo katika maandalizi ya kuhakikisha kwamba inatengeneza mazingira mazuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mafunzo kwa Walimu ni kwamba sasa hivi kuna vyuo 10 ambavyo tumeviangalia na tunaviimarisha maabara zake ili ziweze kutoa mafunzo zaidi kwa masomo ya sayansi. (Makofi)