Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, mafanikio gani yamepatikana kupitia mpango wa umeme jazilizi na lini Kituo cha kupooza umeme cha Uhuru kitafanya kazi?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza: Kwa kuwa ujenzi wa kituo hiki cha umeme umesimama kuanzia mwezi wa Tano mwaka 2022, na kwa taarifa tuliyonayo ni kwamba nguzo zitakazotumika ni za zege: Je, kwanini Serikali isitumie zile nguzo ambazo zimetupwa tangu mwaka 2020 mwezi wa Tano, zitumike kueneza au kusambaza umeme katika maeneo mengine kuliko kuachwa kama zilivyo porini na hata pengine kuzihatarisha na moto na kadhalika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wananchi ambao nguzo hizo za zege zitakazopita wanadai fidia; je, ni lini wananchi hawa watalipwa ili na wenyewe wajiendeleze kiuchumi? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Margaret Sitta kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba design ya awali ilikuwa inatumia nguzo za miti, lakini baada ya maboresho imeonekana ni vema kubadilisha design hiyo na hivyo tutatumia nguzo nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu nimwambie Mheshimiwa Margaret, hizi nguzo tutazitumia kwa kadri ya mahitaji. Vile vile nguzo za kupeleka umeme zinatofautiana kulingana na mahitaji. Zile tulizopeleka kule ni za kupeleka msongo mkubwa wa kilovoti 132, ziko zile za msongo wa kilovoti 33 na ziko zile za distribution za kwenye maeneo yetu ya msongo wa kilovoti 400. Kwa hiyo hizi zilizoko kule tukizipeleka kusafirisha na kusambaza umeme kwa wananchi, tutakuwa tunatumia resource kubwa katika maeneo ambayo siyo yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutapata nguzo nyingine kwa ajili ya kuwapelekea wananchi na hizi zitafanya kazi katika maeneo mengine ambapo zinatakiwa kufanya kazi bila kuathiri mahitaji yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali la pili, nadhani wiki hii kabla haijaisha, wale wataalam ambao walikuwa wanafanya survey kwa ajili ya kulipa compansation, wataanza kuonyesha yale majedwali ya wale wanufaika wa compansation kwa wananchi ili waweze ku-verify na kuona kama ndiyo stahiki na baada ya hapo sasa itarudishwa Wizarani kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kusainiwa na kurekebisha upungufu utakaojitokeza. Tunaamini kwamba katika muda mfupi ujao wa mwezi mmoja au miwili basi fidia zitaanza kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Margaret Sitta awaambie wananchi wawe tayari, wiki hii au mwanzoni mwa wiki inayokuja kwenda kukagua zile fidia ambazo wameandaliwa kwa ajili ya kuhakiki ubora wake.

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, mafanikio gani yamepatikana kupitia mpango wa umeme jazilizi na lini Kituo cha kupooza umeme cha Uhuru kitafanya kazi?

Supplementary Question 2

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri kwamba mradi wa umeme jazilizi kwa kiasi kikubwa sana umefanikiwa, lakini kuna changamoto za upatikanaji wa fedha ili kukamilisha maeneo mengi zikiwemo Kata za Rwanima, Mahina Fumagila pamoja na Kishiri.

Ni lini sasa mkakati wa Serikali kuhakikisha fedha nyingi zinapatikana ili mradi jazilizi uoneshe maana halisi ya kujaziliza kwenye maeneo ambayo hayajapata umeme mpaka leo?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mabula, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu Mheshimiwa Mabula ananufaika na mradi unaoitwa Peri-urban ambao unapeleka umeme katika maeneo ya miji lakini yenye asili ya vijiji. Katika mwaka wa fedha unaokuja imetengwa pesa na eneo lake ni mojawapo ambalo litapelekewa umeme wa kuongezea kwenye yale maeneo ambayo bado hayajapatiwa umeme. Nimwahidi tu kwamba Serikali ya Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan imejikimu na kuamua kupeleka umeme katika kila eneo na pesa imetengwa ya kuanzia itapatikana katika mwaka huu wa fedha unaokuja, na muda sio mrefu ataona wakandarasi wakiwa site. Pia ziko jitihada za ziada za kuendelea kutafuta pesa kwa ajili ya kufikisha kwenye maeneo yote ambayo tunayo.

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, mafanikio gani yamepatikana kupitia mpango wa umeme jazilizi na lini Kituo cha kupooza umeme cha Uhuru kitafanya kazi?

Supplementary Question 3

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza swali dogo la nyongeza kwamba Halmashauri ya Arusha DC inadai fidia ya umeme wa line kubwa inayokwenda Namanga, ni lini sasa Serikali itakamilisha ahadi hii, kwa sababu Halmashauri nyingine zote zimelipwa, imebaki tu Halmashauri Arusha DC?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Lemburis Noah Saputi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba mradi mkubwa anaosema ulikuwa unatoa umeme Iringa kupita Dodoma - Singida kwenda Arusha mpaka Namanga, na kuna maeneo ambayo tayari fidia ilishafanyika. Yalibakia yale maeneo machache ambayo yalikuwa yana matatizo na kutoeleweka kwa nani alipwe fidia au pengine fidia ilitakiwa ilipwe Serikali, wamepewa maeneo mbadala ili wajengewe majengo. Jambo hili tumekubaliana Wizarani kwamba kabla mwaka huu haujaisha, basi yale maeneo ambayo tayari fidia zilishaanza kulipwa yakamilike na pale ambapo pana changamoto kubwa, tujue namna ya kuitatua.

Kwa hiyo, namwahidi kwamba jambo hili tunalifanyia kazi na tutalikamilisha katika muda mfupi ujao.