Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatatua mgogoro wa mpaka kati ya Kambi ya Jeshi 845 Itaka na Wananchi wa Vijiji vya Sesenga na Itewe?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri na niko tayari kuvuta subira kusubiri hiyo tume itakayotuletea majibu ila nilikuwa nina ombi moja kwa Mheshimiwa Waziri, je, tume hiyo itakapomaliza kazi, yuko tayari kwenda na mimi Mbozi kuzungumza na wananchi wa hivyo vijiji na kutoa majibu kwa wananchi hao? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Stergomena Lawrence Tax

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kama nilivyokwishamuahidi Mheshimiwa Mbunge, tumeshazungumza suala hili mara nyingi na nathibitisha tu kwamba, niko tayari kwenda kuongea na wananchi wake. (Makofi)