Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 30 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 266 2022-05-25

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu katika baadhi ya Kata Wilayani Kishapu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Nyangindu Butondo, Mbunge wa Kishapu, Kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imepanga kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika Kata za Busangwa, Itilima, Masanga, Mwakiponya, Mwamalasa, Shagihilu na Talaga ndani ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 ili kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu katika kata hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kata hizo zimejumuishwa katika zabuni inayotarajiwa kutangazwa kabla ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 kukamilika kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.