Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 30 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 259 2022-05-25

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapandisha hadhi Shule ya Sekondari Kalenga iliyopo Kata ya Ulanda kuwa ya kidato cha tano na sita?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga Mbunge wa Jimbo la Kalenga, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maelekezo ya Serikali ni kuwa na Shule ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita katika kila Tarafa zikiwemo Tarafa zilizoko katika Jimbo la Kalenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatafuta fedha katika mwaka 2022/2023 za ujenzi wa bweni la kulalia wanafunzi ili kukamilisha vigezo vya kupandishwa hadhi ya kuwa na Kidato cha Tano na Kidato cha Sita.