Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 53 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 702 2023-06-22

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza: -

Je, upi mpango wa kuwapa mafunzo Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ngazi za Vitongoji, Vijiji, Kata na Wilaya – Pwani?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa Mikoa iliyofanya vizuri katika kuanzisha majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo Jukwaa la Mkoa limeanzishwa kwa mafanikio makubwa hadi kufikia wazo la kuanzisha kiwanda cha vifungashio. Wizara katika bajeti yake ya mwaka 2023/2024 imetenga kiasi cha shilingi milioni 161 kwa ajili ya kujenga uwezo wa majukwaa, ambapo Mkoa wa Pwani utakuwa miongoni mwa Mikoa iliyopo.