Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 696 2023-06-22

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha changarawe barabara ya Mbinga, Kikolo hadi Kihungu ili iweze kupitika wakati wote?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) ajilibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikifanyia matengenezo Barabara ya Mbinga – Kikolo - Kihungu yenye urefu wa kilometa 36 ambapo katika mwaka wa fedha wa 2021, barabara hii ilifanyiwa matengenezo sehemu korofi kwa gharama ya shillingi milioni 150. Aidha, katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, barabara hii imechongwa kwa urefu wa kilometa 30 na kuwekewa changarawe kilometa 14 kwa gharama ya shilingi milioni 247.12.