Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 55 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 720 2023-06-26

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mtwango?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi fedha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Sadan. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya na itapeleka fedha kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mtwango pindi fedha zitakapopatikana.