Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 52 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 690 2023-06-21

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanzisha Tawi la Chuo Kikuu Huria katika Halmashauri ya Ifakara?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali haina mkakati wa kuanzisha Tawi la Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania katika Halmashauri ya Ifakara. Aidha, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimefungua matawi yake katika Makao Makuu ya Mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Mkoa wa Morogoro ambapo wananchi wa Halmashauri ya Ifakara wanapata huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania pia kina vituo vya mitihani kwenye ngazi ya wilaya kwa pale ambapo idadi ya wanachuo ni 50 na kuendelea. Nakushukuru.