Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 40 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 518 2023-06-05

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwalo la Shule ya Sekondari Igwachanya Njombe?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Mabwalo katika Shule za Sekondari nchini. Hata hivyo, natoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kuanza kutenga fedha kupitia Mapato ya Ndani kwa ajili ya ujenzi wa bwalo katika Shule ya Sekondari Igwachanya.