Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 35 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 455 2023-05-29

Name

Kunti Yusuph Majala

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KUNTI Y. MAJALA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa stendi ya Wilaya ya Chemba?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kunti Yusuph Majala, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuwa na Stendi ya Mabasi na kwa kuzingatia umuhimu huo tayari imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 22 na tathmini ya gharama za ujenzi wa stendi hiyo ni takribani milioni 643.82.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuanza na kukamilisha stendi hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba inashauriwa kuandaa andiko la mradi huo ili liweze kutumika kutafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi huo kutoka vyanzo mbalimbali vya fedha.