Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 9 Foreign Affairs and International Cooperation Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 136 2023-09-08

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:-

Je, lini Serikali itafungua Ofisi za Balozi katika nchi za Iran na Pakistan?

Name

Amber. Mbarouk Nassor Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kenneth Ernest Nollo, Mbunge wa Bahi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika hatua ya kufanya tathmini ya kuangalia uwezekano wa kufungua ubalozi katika nchi za Iran na Pakistan. Tathmini hiyo inayofanyika, inajumuisha pamoja na mambo mengine, kuangalia fursa za kiuchumi ambazo nchi yetu itanufaika nazo kwa kuzingatia mwongozo wa Sera ya Mambo ya Nje uliojikita katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi na tija katika matumizi ya fedha za Umma. Taarifa ya Tathmini hiyo itawasilishwa kwa mamlaka husika pindi itakapokamilika.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Tanzania inawakilishwa nchini Iran na Pakistan kupitia ubalozi wetu ulioko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. Ahsante sana.