Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 5 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 64 2023-09-04

Name

Kasalali Emmanuel Mageni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -

Je, lini Serikali itahakikisha tatizo la kutokuwepo mawasiliano ya simu ya uhakika katika maeneo mengi ya Jimbo la Sumve linatatuliwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasasali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Jimbo la Sumve kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefikisha huduma za mawasiliano katika Kata za Bugando, Lyoma, Mwandu, Ngulla na Sumve.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali itafanya tathmini katika Jimbo la Sumve ili kubaini maeneo ambayo bado yana changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano ili yatafutiwe fedha kwa ajili ya kutatua changamoto hizo.